POLISI YASEMA SHABIKI ALIMPULIZIA VUVUZELA NYOSO

Na Paskal Beatus. Bukoba
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kagera, Agustin Ollomi amesema sababu ya mlinzi wa kati wa timu ya Kagera Sugar, Juma Nyoso kumpiga mshabiki ni kukerwa na maneno ya maudhi pamoja na kupuliziwa vuvuzela masikioni.
Tukio hilo lilitokea muda mfupi baada ya kumalizika kwa mchezo wa ligi kati ya Kagera Sugar na Simba ambao Wekundu hao waliibuka na ushindi wa mabao 2-0 uliofanyika kwenye uwanja wa Kaitaba.
Kamanda Ollomi amesema shabiki huyo alishuka jukwaani na kwenda kumpulizia vuvuzela masikioni wakati Nyoso akiwa ametoka kufungwa kitu kilichomfanya kupata hasira.
"Yule shabiki alimfuata Nyoso na kumpulizia vuvuzela masikioni wakati akiwa ana hasira ya kufungwa ndio maana akampiga na kusababisha kuzimia," alisema Kamanda Ollomi.
Taarifa zinasema hali ya shabiki huyo inaendekea vizuri lakini bado yupo hospitali baada ya kuzinduka saa 6 usiku.
Nyoso amefunguliwa shitaka la shambulio wakati shabiki nae amefunguliwa shitaka la kutukana hadharani

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA