Habari njema kwa Wanayanga, kurejea kwa Chirwa na Yondani, Buswita mmh
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga SC jumamosi ijayo (January 27) watakuwa wageni wa Azam FC katika uwanja wa Azam Complex ukiwa ni mchezo wa muendelezo wa ligi kuu Tanzania bara.
Pius Buswita ataukosa mchezo huo, mara ya hapo jana kuoneshwa kadi ya njano ambayo ni ya tatu kwake, lakini ahueni kubwa kwa kikosi cha George Lwandamina ni kurejea kwa mshambuliaji wake Mzambia Obrey Chirwa.
Chirwa na Kelvin Yondani wanarejea uwanjani baada ya kumaliza adhabu zao, Chirwa alifungiwa mechi tatu na Yondani alikuwa na kadi tatu za njano.
Daktari wa mabingwa hao watetezi, Edward Bavu amethibitisha kupatikana kwa huduma ya kinda Yohana Oscar Nkomola aliyeumia hapo jana akieleza kuwa hali yake imetengamaa.