AUBAMEYANG KUTUA ARSENAL
Klabu ya Arsenal inataka kumnunua Pierre Emerick Aubameyang raia wa Gabon kwa kitita cha e60 m, kutoka kwa klabu ya Borrusia Dortmund ya Ujeruman.
Aubameyang (28) ameishawishi Arsenal ambayo hivi karibuni iliondokewa na mshambulizi wake Alexis Sanchez raia wa Chile aliyejiunga na Manchester United.
Sanchez alipishana na Henrick Mkhitaryan ambaye amejiunga na washika bunduki hao wa Amirates, ujio wa Aubameyang hautakuwa rahisi kwani Dortmund hawatamruhusu mpaka pale itakapofanikiwa kumnasa straika mwingine hatari lakini kuna uwezekano wa Olivier Giroud akaangukia kwao