Nyosso amkaribisha Bocco Kaitaba
Na Mwandishi Wetu. Bukoba
Kama umewahi kusikia Juma Nyosso alifunguliwa adhabu ya kufungiwa kucheza soka ndani na nje ya uwanja kwa kipindi cha miaka miwili ujue ni kwa sababu ya John Bocco "Adebayor".
Sikia ilikuwa hivi, Nyosso alikuwa anaichezea Mbeya City akiwa nahodha, na John Bocco naye akiichezea Azam Fc naye nahodha, basi ilipigwa mechi uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi.
Nyosso alimdhalilisha Bocco kwa kumwingiza kidole makalioni, hapo ndipo TFF iliponfungia kwa miaka mitatu, na mwaka jana alifunguliwa ndipo alipojiunga na Kagera Sugar na Jumatatu kwa mara ya kwanza Nyosso anakutana tena na Bocco.
Mambo Uwanjani iliwasiliana kwa simu na beki huyo wa zamani wa Ashanti United, Simba Sc na Coastal Union na kusema anamkaribisha Bocco