Yanga yaichinja Azam, Chamazi

Na Ikram Khamees. Dar es Salaam

Hatimaye ule ubishi wa nani mbabe kati ya mabingwa wa Afrika mashariki na kati, maarufu kombe la Kagame Azam Fc na mabingwa wa Tanzania bara Yanga Sc umemalizika kwa Yanga Sc kuilaza Azam Fc mabao 2-1 uwanja wa Azam Complex, Chamazi, mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Azam Fc inayonolewa na Mromania, Aristica Cioaba, ilitangulia kupata bao la uongozi lililofungwa na mshambuliaji wake chipukizi, Shaaban Iddy Chilunda aliyepasiwa krosi na Mzimbabwe Bruce Kangwa.

Baada ya kuingia goli hilo, Yanga walicharuka na kulishambulia lango la Azam kama nyuki na kufanikiwa kusawazisha kupitia Obrey Chirwa aliyepasiwa na Ibrahim Ajibu, kabla ya kwenda mapumziko Yanga wakaongeza bao la pili lililofungwa na Gardiel Michael kwa shuti kali.

Hadi mapumziko Yanga walikuwa mbele, kipindi cha pili kila timu ilishambulia kwa zamu lakini mwisho Yanga wakaibuka wababe na kufikisha pointi 28 wakiendelea kushikilia nafasi ya tatu, Azam wanabaki na pointi zao 30.

Mchezaji Salum Abubakar "Sure Boy" alipewa kadi nyekundu baada ya kumpiga makusudi Hassan Kessy, matokeo mengine ya Ligi Kuu Bara ni kama ifuatavyo, Mbeya City 0 Mtibwa Sugar 0, Kagera Sugar 0, Lipuli 0 na Mwadui 2 Njombe Mji 2

Wachezaji wa Yanga wakishangilia ushindi wao leo dhidi ya Azam Fc 

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA