KIPA WA SIMBA NA YANGA AFARIKI BURUNDI
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Mlinda mlango wa zamani wa Simba na Yanga na African Lyon, Ismail Suma amefariki dunia huko Bujumbura nchini Burundi.
Kwa mujibu wa kaka wa marehemu, Salum Athuman amesema kuwa Suma amefariki dunia baada ya kuugua maradhi ya Ini.
Kipa huyo aliyeibukia Kariakoo Lindi na kujiunga na Yanga Sc mwaka 2000 ambapo aling' ara na kujiunga na mahasimu wao Simba kabla ya kujiunga na African Lyon wakati huo ikiitwa Mbagala Market aliugua kwa muda mrefu kabla ya umauti kumfika.
Suma (Pichani wa kwanza kushoto)
alienda Burundi baada ya kuondoka DR Congo alikokuwa anacheza soka la kulipwa, mazishi ya mchezaji huyo yatafanyika Burundi baada ya familia yake kushindwa kuuleta mwili Tanzania