Man United klabu tajiri duniani
Manchester United imeongoza orodha ya klabu 20 tajiri zaidi duniani kwa mwaka wa pili mfululizo na mara ya 10 kwa jumla , kulingana na kampuni ya Deloitte.
Mbali na msimu wa 2016-17 jumla ya mapato ya klabu hizo 20 imeongezeka kwa asilimia 6 hadi €7.9bn (£6.97bn), ikiwa ni rekodi mpya.
Real Madrid ilioongoza kwa miaka 11 ilikuwa ya pili na Barcelona ikawa ya tatu.
Kulikuwa na rekodi ya klabu 10 za Uingereza katika orodha hiyo ya 20 bora.
Orodha hiyo inaangazia mapato yaliopatikana na haiangazii madeni ya vilabu.
•1. Manchester United: €676.3m
•2. Real Madrid: €674.6m
•3. Barcelona: €648.3m
•4. Bayern Munich; €587.8m
•5. Manchester City: €527.7m
•6. Arsenal: €487.6m
•7. Paris Saint Germain: €486.2m
•8. Chelsea: €428m
•9. Liverpool: €424.2m
•10. Juventus: €405.7m
Duru: Deloitte, Mapato ya msimu wa 2016-17