BEKI MPACHIKA MABAO APATA ULAJI KENYA

Na Mwandishi Wetu. Kenya

Beki Mtanzania mwenye sifa ya kupachika mabao aliyepata kuchezea Azam Fc, Coastal Union na Majimaji ya Songea, Tumba Lyi Sued amejiunga na timu ya Wazito Fc ya nchini Kenya kwa mkataba wa miaka miwili.

Sued ndiye beki aliyeanza kusifika kwa upachikaji magoli, ameamua kujiunga na timu hiyo ikiwa ni sehemu ya kutimiza ndoto yake ya kucheza soka nje ya Tanzania.

Mchezaji huyo aliyesajiliwa na Majimaji mwanzoni mwa msimu huu baada ya kuachana na Coastal Union ya Tanga, amefurahia kutua Wazitp Fc ya Kenya na kudai ni hatua nzuri aliyoifikia kujiunga na timu hiyo.

Tumba Sued ambaye aliibuliwa na kulelewa na kituo cha Azam Academy kilichopo Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam anaungana na Watanzania wengine wanaosakata soka la kulipwa nchini Kenya

Tumba Sued Lui (Kushoto) amesajiliwa na timu ya Wazito

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA