Yanga na Azam waambulia milioni 28
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam
Pambano la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya klabu bingwa Afrika mashariki na kati, Azam Fc na mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga Sc limeingiza shilingi milioni 28 za Kitanzania.
Mchezo huo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa uwanja wa Azam Complex, juzi Jumamosi Chamazi na Yanga kushinda mabao 2-1 uliingiza kiasi hicho cha pesa ambacho kinatajwa ni kidogo.
Katika mchezo huo Azam ilitangulia kupata bao katika dakika ya tatu na mshambuliaji wake chipukizi Shabani Chilunda, lakini Yanga wakasawazisha kupitia Obrey Chirwa na Gadiel Michael Mbaga kwa shuti kali