NI VITA YA WABABE NA VIBONDE WA SIMBA LEO CHAMAZI

#Michezo: NI VITA YA WABABE NA VIBONDE WA SIMBA LEO CHAMAZI.

Michuano ya kombe la Azam Sports Federation Cup (ASFC) maarufu FA Cup leo inaendelea kushika kasi katika viwanja tofauti hapa nchini, mtanange mkali na wa kusisimua utapigwa pale Azam Complex, Chamazi ikizikutanisha Green Warriors ya Mwenge jijini na Singida United ya mkoani Singida.

Ugumu wa mchezo huo unakuja pale unapozikutanisha timu mbili ambazo zina rekodi tofauti, Green Warriors hawatasahaulika na wapenzi wa soka baada ya kuiondosha na kuivua ubingwa wa michuano hiyo Simba.

Katika mchezo uliowakutanisha na Simba, ulimalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1 na walipoenda kwenye penalti Green Warriors wakaibuka wababe kwa mikwaju 5-4.

Singida United nao wanaingia uwanjani wakiwa vibonde wa Simba baada ya kulazwa mabao 4-0 mchezo wa Ligi Kuu Bara na hapo ndiyo kutatoa mbabe wa kweli hii leo.

Mechi nyingine za michuano hiyo itapigwa kama ifuatavyo.

Majimaji Rangers vs Mtibwa Sugar Ilulu Lindi, Majimaji Fc vs Ruvu Shooting, Majimaji Stadium Songea, Njombe Mji Fc vs Rhino Rangers, Kiluvya United vs JKT Orjolo, Mabatini Pwani, Pamba Fc vs Stand United, CCM Kirumba, Mwanza.

Nyingine ni kati ya Tanzania Prisons vs Burkina Faso, Sokoine Mbeya wakati mchezo kati ya KMC na Toto Africans sasa utapigwa Februali 7 mwaka huu Azam Complex, Chamazi

Kikosi cha Green Warriors kinacheza na Singida United leo

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA