Simba yaipashia Kagera Sugar
Na Mwandishi Wetu. Bukoba
Unakumbuka ule mchezo wa msimu iliopita kati ya Simba Sc na Kagera Sugar ambao ulimalizika kwa Simba kufungwa mabao 2-1 mchezo wa Ligi Kuu Bara duru la lala salama.
Kipigo kile kiliwafanya Simba wakose ubingwa wa Bara uliokwenda kwa Yanga, sasa timu hizo zinakutana tena Jumatatu ya wiki ijayo katika uwanja wa Kaitaba uliopo mkoani Kagera.
Leo hii wachezaji wa Simba wakiwa chini ya kocha msaidizi Masoud Djuma, waliipashia Kagera Sugar katika uwanja wa Tengamano Seminal School kabla ya kesho kupasha katika uwanja wa Kaitaba, Simba ndio vinara wa Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi 29