Tambwe, Maftah wamtetea Nyoso, Waziri wa Ulinzi aonya

Na Saida Salum. Dar es Salaam

Kitendo kilichofanywa na beki wa Kagera Sugar, Juma Nyoso cha kumpiga shabiki wa klabu ya Simba hadi kuzimia, kimeungwa mkono na baadhi ya wachezaji na kukosolewa pia.

Kipa wa zamani wa Villa Squad, Zimamoto ya Zanzibar na timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys, Kitwana Tambwe ameunga mkono kitendo cha Nyoso kumpiga shabiki huyo kwani hata yeye amewahi kumpiga kichwa shabiki aliyemzomea baada ya kufungwa.

Lakini beki wa zamani wa Yanga na Simba, Amir Maftah yeye amelaani vikali kitendo cha Nyoso kumpiga shabiki lakini akadai hata yeye alipokuwa na Yanga waliwahi kumpiga shabiki mjini Morogoro hadi akazimia kisa tu aliwatukana.

Ila beki wa zamani wa Yanga na APR ya Rwanda, Hamis Yusuf "Waziri wa ulinzi" ameonya vitendo kama hivyo vya kupiga mashabiki kwani amedai siyo vizuri, Yusuf amedai mashabiki ndio wamekuwa wakiwaaapoti wachezaji hivyo kuwapiga si haki

Juma Nyoso ametetea na wachezaji wenzake

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA