ISMAIL SUMA AZIKWA BURUNDI
Na Mwandishi Wetu.
Mlinda mlango wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Ismail Suma amezikwa jana mjini Bujumbura, Burundi baada ya familia yake kushindwa kuusafirisha mwili nchini Tanzania.
Suma aliyezichezea Kariakoo Lindi, Yanga, Simba na African Lyon, amezikwa jana katika makaburi ya Bujumbura, Burundi kufuatia kufariki dunia kwa maradhi Ini.
Kipa huyo aliondoka Tanzania na kwenda DR Congo kucheza soka la kulipwa ambapo pia aliondoka na kuelekea Burundi pia kucheza soka la kulipwa ambapo mauti yakamfika.
Baadhi ya wachezaji wenzake aliocheza nao nchini Tanzania wameonyesha kusikitishwa na kifo cha kipa huyo na kuliomba Shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) kusaidia kuuleta mwili nyumbani Tanzania kwa mazishi