Yanga, Azam na Singida United zaingia vitani FA Cup

Na Exipedito Mataruma. Mbeya

Baada ya kukamilika kwa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, uhondo umehamia katika michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) maarufu FA Cup ambapo miamba Yanga, Azam na Singida United zitaingia vitani kesho Jumatano na keshokutwa Alhamisi.

Mabingwa wa soka nchini Yanga Sc wao watasafiri hadi mkoani Mbeya ambapo watachuana na timu ya Ihefu Fc katika uwanja wa Sokoine, lakini klabu bingwa Afrika mashariki na kati Azam Fc wao wataifuata Shupavu Fc katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Pambano lingine la kusisimua litakuwa pale Azam Complex, Chamazi likihusisha kigogo Singida United dhidi ya wenyeji wao Green Warriors, huo nao unatajwa kuwa mchezo mgumu kwakuwa vijana wa Green Warriors waliiondoa Simba na kuinyang' anya ubingwa ilioutwaa mwaka jana

Yanga watacheza na Ihefu Fc mjini Mbeya

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA