SINGIDA UNITED YAFUFUKIA KWA PRISONS
Na Mwandishi Wetu. Singida
Wenyeji Singida United jioni ya leo wameamka usingizini baada ya kuichakaza Tanzania Prisons bao 1-0 mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara uliopigwa uwanja wa Namfua Singida.
Goli ambalo limeibeba Singida United limefungwa na mshambuliaji wake Mzambia Elinyesia Sumbi na kuifanya timu hiyo kukwea hadi nafasi ya nne.
Vijana wa Singida United wanaonolewa na Mholanzi Hans Van der Pluijm wamefikisha pointi 27 wakiwa nyuma ya Yanga yenye pointi 28, Singida sasa inajiandaa kucheza na Mwadui hapo hapo Namfua mwishoni mwa wiki ijayo