Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Desemba, 2017

Yanga chali tena kwa Mbao

Picha
Na Paskal Beatus. Mwanza Mabingwa wa soka Tanzania bara Yanga Sc jioni ya leo imeendelea kuwa mteja kwa vijana wa Mbao Fc baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-0 mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Vijana wa Mbao wakicheza kandanda safi na kulisakama lango la Yanga lakini hadi mapumziko timu zote hazikufungana hata bao, kipindi cha pili Mbao Fc waliliandama lango la Yanga kama nyuki na kuandika goli la kwanza lililofungwa na Habibu Haji Kiyombo kunako dakika ya 53 kabla ya dakika ya 68 kuongeza bao la pili. Kwa kipigo hicho Yanga wanashuka hadi nafasi ya nne ikiipisha Singida United ambayo jioni ya leo imeichapa Njombe Mji mabao 3-0 uwanja wa Sabasaba mjini Njombe, Singida imefikisha pointi 24 huku Yanga ikibaki na pointi 21 na kesho inaanza safari ya kuelekea visiwani Zanzibar kushiriki Mapinduzi Cup Mbao Fc imeendeleza ubabe kwa Yanga

MTANGAZAJI MAARUFU WA MICHEZO AFARIKI DUNIA

Picha
Na Saida Salum. Dar es Salaam Tasnia ya habari leo imepatwa na msiba mzito baada ya aliyekuwa mtangazaji maarufu wa kipindi cha michezo cha redio Uhuru, Limonga Justine Limonga kufariki dunia. Marehemu alikuwa akitangaza kipindi cha michezo kinachorushwa na redio Uhuru kuanzia saa 1:00 usiku hadi saa 1:30 usiku. Marehemu aiingia kwenye utangazaji baada ya kuachana na kutuma salamu ambayo ilimsukuma hadi kuwa mtangazaji, bado tutaendelea kuwajuza taarifa za msiba wake kama mazishi yatafanyika lini na wapi. Kwa niaba ya Mtendaji mkuu wa Mambo Uwanjani inawapa pole wafiwa kwa msiba huo pamoja na Radio Uhuru Fm Limonga Justine Limonga amefariki dunia

KITAELEWEKA LEO YANGA NA MBAO CCM KIRUMBA

Picha
Na Paskal Beatus. Mwanza Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara inaendelea tena leo kwa mitanange miwili kupigwa katika viwanja viwili tofauti, lakini nchi itasimama kwa muda pale jijini Mwanza kwenye uwanja wa CCM Kirumba wakati Mbao Fc itakapowaalika mabingwa watetezi Yanga Sc. Kocha wa Mbao Fc, Mrundi, Etiene Ndayiragije ametamba kuendeleza kichapo kwa Yanga kwani msimu uliopita Mbao iliifunga Yanga bao 1-0 kwenye Ligi Kuu bara na pia kwenye kombe la FA, hivyo leo tena Mbao anashinda, lakini kocha msaidizi wa Yanga Shadrack Nsajigwa "Fuso" amesema thubutuu!. Nsajigwa beki wa zamani wa kikosi hicho pamoja na timu ya taifa, Taifa Stars ametamba kulipiza kisasi katika mchezo wa leo huku akidai ilichokipata Reha Fc ndicho itakipata Mbao Fc leo na shahidi ya hayo ni dakika 90 Yanga wanacheza na Mbao Fc leo

JKU YAISHIKISHA ADABU ZIMAMOTO

Picha
Na Mwandishi Wetu. Zanzibar Timu ya Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) jioni ya leo imefufua matumaini ya kusonga mbele katika michuano ya kombe la Mapinduzi baada ya kuilaza timu ya Jeshi la Zimamoto bao 1-0 mchezo wa kwanza kundi B na kujikusanyia pointi tatu muhimu. Bao lililoipa ushindi JKU lilifungwa mapema kabisa na Salum Musa Bajaka katika dakika ya kwanza kabisa kuanza kwa pambano hilo, mechi nyingine ya pili inaendelea kupigwa usiku huu kati ya Mlandege na Taifa Jang' ombe uwanja huo huo wa Amaan, Zanzibar. Michuano hiyo itaendelea tena kesho kwa kundi A, Azam Fc vs Mwenge utaanza saa 10:00 na kufuatiwa na mchezo mwingine kati ya Jamhuri na URA ya Uganda ambayo ni timu mwalikwa Kikosi cha JKU kimeifunga Zimamoto 1-0

SIMBA YACHANUA MAKUCHA NA KUIPALULA NDANDA FC

Picha
Na Ikram Khamees. Mtwara Simba Sc jioni ya leo imefufua tena mbio zake za ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara baada ya kuilaza Ndanda Fc "Wanakuchele" nyumbani kwao katika uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara. Hadi mapumziko timu hizo hazikufungana hata bao, kipindi cha pili Simba walikuja na kasi mpya na kulisakama lango la Ndanda kama nyuki na kuweza kujipatia mabao hayo mawili yote yakifungwa na mshambuliaji John Raphael Bocco "Adebayor" dakika ya 52 na 56. Kwa ushindi huo Simba inarejea kileleni ikifikisha pointi 26 sawa na Azam Fc ila inazidi kwa magoli ya kufunga, Lipuli Fc ya Iringa ilikubali kichapo nyumbani baada ya kufungwa 1-0 na Tanzania Prisons uwanja wa Samora mjini Iringa, Mtibwa Sugar nayo ikicheza nyumbani Manungu Complex, Morogoro imeifunga 2-1 Majimaji ya Songea uwanja wa Manungu Complex, Morogoro Simba imeifunga Ndanda 2-0 leo

Wanachama Yanga Mwanza wawajaza noti wachezaji kuiua Mbao kesho

Picha
Na Paskal Beatus. Mwanza Wanachama na matawi yote wa klabu ya Yanga jijini Mwanza wamechangishana kiasi cha fedha shilingi Laki tisa na elfu thelasini na kumkabidhi kaimu mwenyekiti wa klabu hiyo Clement Sanga ili awapatie wachezaji wao kama motisha ya kuisambaratisha timu yao ya Mbao Fc ambao watakutana nao kesho Jumapili mchezo wa Ligi Kuu bara uwanja wa CCM Kirumba Mwanza. Wanachama hao wamekutana leo na kufanya kikao chao kilichoudhuriwa pia na kaimu mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga, na katika maadhimio hayo wanachama hao wameahidi kuchangishana fedha ili kusaidia usajili wa wachezaji kwa msimu ujao. Yanga kwa sasa haina mfadhili hasa baada ya kujiuzuru kwa mwenyekiti wake Yusuf Manji ambaye pia alikuwa akijitolea kuisaidia timu hiyo, kesho Yanga itachuana na Mbao na tayari imewasili jijini humo kwa ndege ikitokea Dar es Salaam, ligi hiyo pia itaendelea kwa mchezo mwingine kati ya Njombe Mji na Singida United uwanja wa Sabasaba mjini Njombe Wanachama wa Yanga kutoka matawi ...

Simba kurejea kileleni leo?

Picha
Na Ikram Khamees. Mtwara Wekundu wa Msimbazi,Simba Sc jioni ya leo itakuwa ugenini kwa Ndanda Fc uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara, Simba iliwasili mjini Mtwara Alhamis ikitokea Dar es Salaam ambako ina kumbukumbu ya kuvuliwa ubingwa wa kombe la FA. Mchezo huo wa leo utakuwa mgumu kutokana na kila timu kutaka pointi tatu muhimu, wenyeji Ndanda wao walibadili nahodha kuelekea mchezo huo ambapo jukumu zima alikabidhiwa mshambuliaji Jacob Masawe na kiungo wa zamani wa Yanga, Salum Telela. Simba nao wameamua kubadili benchi la ufundi, ikimtoa Mcameroon, Joseph Omog na kumpa Mrundi, Masoud Djuma, endapo Simba itashinda mchezo huo itarejea kileleni kwani jana usiku Azam Fc ilishinda mabao 3-0 na kukamata usukani Simba wanaweza kurejea kileleni leo

Azam FC yapaa kileleni, Mghana wake ang' ara

Picha
Na Saida Salum. Dar es Salaam Klabu bingwa ya soka Afrika mashariki na kati, Azam FC imekamata usukani wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara baada ya kuilaza Stand United mabao 3-0 mchezo ukimalizika usiku huu katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam. Kwa ushindi huo mnono Azam inakaa kileleni mwa msimamo wa ligi, ikifanikiwa kufikisha alama 26 ikicheza mechi 12, Simba SC ndio walikuwa wakiongoza ligi hiyo, lakini inaweza kurejea kileleni endapo itashinda dhidi ya Ndanda FC. Mabao ya Azam FC katika mchezo huo wa leo yamefungwa na Salmin Hoza, Benard Athur na Bruce Kangwa, ligi hiyo itaendelea kesho kwa michezo mitatu ambapo Mtibwa Sugar itawaalika Majimaji, Ndanda na Simba, wakati Lipuli ya Iringa itakuwa mwenyeji wa Prisons Benard Athur raia wa Ghana amefunga goli la pili Azam ikishinda mabao 3-0

MLANDEGE YAILAZA JKU 2-1, MWENGE NAO WATAKATA

Picha
Na Mwandishi Wetu. Zanzjbar Timu ya Mlandege mchana wa leo imeanza vema michuano ya Mapinduzi baada ya kuilaza timu ngumu ya JKU mabao 2-1 uwanja wa Amaan, Zanzibar huo ulikuwa mchezo wa ufunguzi. Mlandege ilicheza vizuri na kujipatia mabao yake kupitia kwa Khamis Abuu dakika ya 18 na Abubakar Ame (Luiz) dakika ya 60, goli la JKU limefungwa na Khamis Abdallah dakika ya 34. Timu ya Mwenge kutoka Pemba iliwachapa ndugu zao Jamhuri kwa bao 1-0 lililofungwa na Ally Salim Bajaka kunako dakika ya 31, mechi nyingine inapigwa usiku huu kati ya Taifa Jang' ombe na Zimamoto, michuano hiyo itaendelea tena kesho ambapo Zimamoto watacheza na JKU na Taifa Jang' ombe na Mlandege Michuano ya Mapinduzi imeanza leo uwanja wa Amaan, Zanzibar

AZAM FC KUISHUSHA KILELENI SIMBA LEO?

Picha
Mrisho Hassan. Dar es Salaam Klabu bingwa Afrika mashariki na kati, Azam FC usiku wa leo inaikaribisha Stand United katika uwanja wake wa Azam Complex uliopo Chamazi mjini Dar es Salaam, mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara. Endapo Azam FC itaibuka na ushindi wa aina yoyote dhidi ya wapiga debe hao wa Stand, basi itakuwa imeishusha kileleni Simba na kuongoza ligi hiyo, Azam ina pointi 23 sawa na Simba ila imezidiwa magoli ya kufunga. Mechi nyingine za ligi hiyo zitapigwa kesho hadi keshokutwa, kesho Desemba 30 mwaka 2017 Lipuli itaialika Tanzania Prisons uwanja wa Samora mjini Iringa wakati Mtibwa Sugar ikiwakaribisha Majimaji uwanja wa Manungu Complex. Ndanda FC nao watawakaribisha Simba SC uwanja wa Namgwanda Sijaona mjini Mtwara wakati siku ya Jumapili Desemba 31, 2017 Njombe Mji itakuwa mwenyeji wa Singida United, Sabasaba Stadium mjini Njombe Mbao FC nao itakuwa mwenyeji wa Yanga SC, CCM Kirumba Mwanza, Januari 1, 2018 Mbeya City itaikaribisha Kagera Sugar uwanja wa Sok...

UHURU KENYATA AMTUMIA SALAMU ZA PONGEZI GEORGE WEAH

Picha
Rais wa jamhuri ya watu wa Kenya, Uhuru Kenyata amemtumia salamu za pongezi Rais mteule wa Liberia, George Opong Weah kwa kuchaguliwa kuwa rais mpya wa taifa hilo la Afrika magharibi katika uchaguzi wa kidemokrasia uliofanyika mwezi huu. Weah alimshinda mpinzani wake Joseph Boakai ambaye ni makamu wa rais wa serikali inayomaliza muda wake chini ya rais Helen Johnson Serleaf. Katika salamu zake, Kenyata ambaye naye alishinda kiti cha urais hivi karibuni, amemsifu Weah kwa ushindi huo na kumtaka aliongoze vema taifa hilo lililowahi kumwaga damu kwa kupigana vita ya wenyewe kwa wenyewe. Weah anatarajia kuapishwa Januari Mwakani, na pia amewahi kuwa mwanasoka bora wa dunia, akizichezea timu mbalimbali barani Ulaya kama Monaco ya Ufaransa, Ac Milan ya Italia, Man City na Chelsea za England kisha El Jazira ya Uarabuni George Weah ametumiwa salamu za pongezi kwa kushinda Urais wa Liberia

Mwinyi Haji kutimkia AFC Leopards

Picha
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam Mlinzi wa kushoto wa mabingwa wa soka nchini, Yanga SC, Mwinyi Haji Mngwali ameuandikia barua uongozi wa Yanga akitaka imwachilie akajiunge na AFC Leopards ya Kenya baada ya kuchoka kukalia benchi, Mwinyi alitamba katika michuano ya kombe la Chalenji iliyofanyika hivi karibuni nchini Kenya. Mwinyi alikuwa na kikosi cha timu ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes ambacho kilimaliza katika nafasi ya pili, beki huyo amekuwa apewi nafasi ya kucheza katika kikosi cha Yanga na Gerdiel Michael aliyesajiliwa kutoka Azam FC msimu huu ndiye amekuwa akianza katika kikosi cha kwanza cha mabingwa hao wa Bara. Lakini kwa uwezo mkubwa aliouonyesha Mwinyi katika michuano ya Chalenji na kuivutia timu ya AFC Leopards inayoshiriki Ligi Kuu ya Kenya (KPL) ambapo imetangaza kumsajili, hivyo beki huyo ameandika barua kwa waajiri wake waweze kumwachilia akajiunge na timu hiyo. Mwinyo Haji Mngwali anataka kuondoka Yanga

Staa Wetu

Picha
Joseph Marius Omog. Shujaa aliyefia vitani. Na Prince Hoza SIKUWEZA kuamini pale niliposikia kocha mkuu wa Simba SC, Mcameroon Joseph Marius Omog amefutwa kazi kuinoa timu hiyo, sikuamini kabisa taarifa hiyo ya kufutwa kazi, taarifa ilianzia kusambaa kwenye mitandao ya kijamji mchana. Mitandao ya kijamii siku hizi haiaminiki sana kwakuwa kuna watu wamekuwa wakisambaza uongo, na ndio maana watu wenye heshima zao hawataki kuamini haraka taarifa zinazosambazwa mitandaoni, ilikuwa haraka kuamini Abdallah Kibaden "King" kuwa amefariki dunia. Kuna watu walieneza uzushi huo kuwa Kibaden amefariki wakati si kweli, ndivyo nilivyoshindwa kuamini kama Omog amefutwa kazi Simba. Lakini nilikuja kuamini pale niliposikia Afisa Habari, Haji Manara akithibitisha, Omog alitimuliwa kazini baada ya Simba kutolewa katika michuano ya Azam Sports Federation Cup, (ASFC), maarufu kombe la FA. Wekundu hao wa Msimbazi walifungwa na timu ya daraja la pili ya Green Warriors kwa mabao 4-3 yaliyotoka...

Mourinho amkataa Griezmann, Barcelona wachekelea

Picha
Manchester United Hawana Mpango tena  wa kutaka kumuongeza Mfaransa Antoine Griezmann baada ya kocha Mwenye Maneno Mengi Mreno Josee Mourinho kudai hajaridhishwa na kiasi anachouzwa nyota huyo anaekipiga kunako Klabu ya Atletico Madrid ya Spain. Taarifa kutoka Gazeti la Marca zinasema Mourinho hajashawishika na kiwango kikubwa cha Fedha anachouzwa Mfaransa huyo ili aweze kutua kwenye Premier League na kusisitiza hata msimu uliopita Board ndio ilikuwa imeshawishika zaidi kutaka kumsajili. Baada ya mwaka kumalizika Atletico Madrid watakuwa wamemaliza adhabu yao ya kutokusajili na Tayari watakuwa na Mshambuliaji wao kwa Mara nyingine Diego Costa (Burrega)Kitendo kinachoonyesha kuwa Griezmann ataondoka ndani ya klabu kitendo kitakachofungua Milango kwa Barcelona kuona namna ya kumpata Antoine Griezmann ambae anapatikana kwa kitika cha €100 Million (£88). Hata hivyo Barcelona wanabaki njia panda kuhusu nani asajiliwe Kati ya Antoine Griezmann au Mbrazili Phillipe Coutinho baada ya ku...

Ndanda wabadili nahodha kisa Simba

Picha
Na Mwandishi Wetu. Mtwara Benchi la ufundi la Ndanda SC limefanya Mabadiliko ya Nahodha wa Klabu ambapo awali Nahodha Mkuu alikuwa Rajabu Zahiri aliyehamia Ruvu shooting Na alikuwa akisaidiwa Na William Lucian Na Jeremia Kisubi. Kwa Sasa Nahodha Mkuu atakuwa Jacob Masawe akisaidiwa Salum Telela, Jeremia Kisubi na Hemed Khoja. Haya ni Mabadiliko ya kawaida kufanywa Na Benchi la Ufundi Kwa Majibu wa Kocha Mkuu Malale Hamsini, Ndanda inakabiliwa na mchezo wake wa Ligi Kuu Bara dhidi ya vinara Simba SC, Jumamosi katika uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara. Jacob Masawe nahodha mpya Simba

MAPINDUZI CUP KUANZA KUTIMUA VUMBI KESHO

Picha
Na Mwandishi Wetu. Zanzibar Michuano ya kombe la Mapinduzi inatarajia kuanza kutimua vumbi kesho katika uwanja wa Amaan, Zanzibar kwa mechi tatu, timu za Mlandege FC na JKU zitaanza kuchuana kuanzia saa 8:00 mchana, ikifuatiwa na mechi nyingine kati ya Jamhuri na Mwenge zote za Pemba mchezo wao ukipigwa saa 10:00 jioni. Mchezo mwingine utapigwa usiku kuanzia saa 2:15 kati ya Taifa Jang' ombe na Zimamoto, michuano hiyo inayoshirikisha pia miamba ya soka nchini Simba na Yanga pamoja na Singida United. Michuano hiyo inayoratibiwa na chama cha soka Zanzibar, (ZFA) itaendelea kutimua vumbi, lakini Siku ya Jumapili Azam FC itaumana na Mwenge, wakati Singida United itacheza na Zimamoto, siku ya Jumanne Simba itacheza na Mwenge wakati Yanga itachuana na Mlandege. Kikosi cha Mlandege FC kitafungua dimba Mapinduzi Cup

RAIS TFF APIGA MARUFUKU MASHINDANO YA NDONDO MCHANGANI

Picha
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu nchini, (Tff) Wallace Karia amepiga marufuku mashindano yote yasiyo rasmi mitaani maarufu kama ndondo hasa yale ya kombe la mbuzi au ng' ombe. Karia ameyasema hayo leo wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba mpya baina ya Tff na kampuni ya Macron ambayo itatengeneza jezi za timu zote za taifa, Rais Karia amewataka watu wanaodhamini mashindano ya ndondo mchangani hasa madiwani, wabunge nk kujitolea udhamini huo kwa timu za majimboni mwao badala ya kuanzisha mashindano hayo ambayo hayatambuliki na Tff. Kwa kauli hiyo ya kiongozi huyo wa soka nchini, michezo ya ndondo inayochangia kukuza na kuinua viwango vya soka kwa wachezaji wengi hapa nchini sasa haitafanyika tena, tayari baadhi ya wanamichezo wameanza kupingana na kauli hiyo wakimtuhumu Rais huyo wa Tff kwa kudai amekurupuka Wallace Karia amepiga marufuku mashindano ya ndondo mchangani

LEONARDA AFUNIKA VIDEO YA HAMOSNOTA

Picha
Na Saida Salum. Dar es Salaam Video queen anayechipukia katika kiwanda cha muziki bongo, Leonarda Wolper ameweza kuwa kivutio kwenye video ya msanii wa bongofleva, Hamosnota. Watu waliotazama video hiyo wamesema mwanadada huyo ametokelezea vizuri kuliko hata video queen wa wimbo huo, Leonarda ameuza sura mara moja katika wimbo wa Pole wa msanii huyo lakini amefunika mno. Leonarda pia ni muigizaji na anatarajia kuonekana katika filamu mpya inayotarajia kutoka ya msanii Elia Daniel, mbali na kushiriki katika video ya Hamosnota, Leonarda ameonekana pia kwenye wimbo wa Lava Lava Leonarda Wolper amefunika katika video ya Hamosnota kupitia wimbo wa Pole

Hatimaye George Weah awa Rais wa Liberia

Picha
Tume ya taifa ya nchini Liberia imemtangaza rasmi mwanasoka wa zamani wa AC Milan na Mwafrika pekee kushinda tuzo ya Ballon' D'Or, George Opong Weah baada ya kupata ushindi mkubwa kwenye uchaguzi wa taifa hilo. Weah anakuwa Rais wa 25 na amemshinda Joseph Boakai ambaye alikuwa makamu wa Rais wa nchi hiyo, mwanasoka huyo bora wa dunia aliyepata pia kuzichezea Monaco, Marseile zote za Ufaransa, Inter Milan ya Italia, Manchester City na Chelsea zote za England, ameibuka mshindi katika majimbo 12 kati ya 15. Aidha Weah ambaye aliwahi kuja nchini Tanzania akiwa na timu ya taifa ya Liberia, amewashukuru wananchi wa taifa hilo waliomchagua na kuahidi kuleta mapinduzi makubwa, Weah aliwahi pia kushinda urais wa nchi hiyo lakini matokeo yalifutwa na mahakama George Weah Rais mpya wa Liberia

Nitafanya mambo makubwa Ndanda- Ngasa

Picha
Na Mwandishi Wetu. Mtwara Mshambuliaji Mrisho Khalfan Ngasa amesema atafanya mambo makubwa akiwa na kikosi chake kipya cha Ndanda FC ya mkoani Mtwara alichojiunga nacho katika usajili wa dirisha dogo la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara. Ndanda inakutana na Simba Jumamosi ijayo katika uwanja wa Nangwanda Sijaona mchezo wa Ligi Kuu bara na Mrisho Ngasa amesema mchezo huo utakuwa muhimu kwake kwani wapenzi na mashabiki wa Ndanda wanampa matumaini makubwa ya kufanya vizuri akiwa na kikosi hicho. Ngasa amefunguka kuwa anajisikia furaha kucheza Ndanda na hata kiwango chake anaamini kinaweza kurejea kama zamani, amewataka Wanamtwara kujitokeza kwa wingi na kuiunga mkono timu yao ya nyumbani itakavyotoa ushindani kwa Simba iliyojeruhiwa. Simba ilitolewa katika michuano ya FA baada ya kufungwa mabao 4-3 kwa mikwaju ya penalti kufuatia sare ya bao 1-1 dhidi ya Green Warriors ya daraja la pili, matokeo yaliyosababisha kufukuzwa kazi kwa kocha wao mkuu, Mcameroon, Joseph Marius Omog. Mrish...

Zanzibar noma kotekote, yatwaa ubingwa wa soka la ufukweni

Picha
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam Kama unadhani timu ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes ni wabaya kwenye soka la kawaida kama ilivyofanya kweli huko Kenya kwenye michuano ya Chalenji kwa kuingia fainali, basi jana kikosi cha timu ya taifa ya Zanzibar cha soka la ufukweni kimetwaa ubingwa wa michuano ya Copa Dar es Salaam baada ya kuishinda timu ya taifa ya Malawi mabao 3-2 kwenye mchezo wa fainali. Mchezo huo ulifanyika katika fukwe za Coco Beach Dar es Salaam na Zanzibar ilionekana kutakata katika michuano hiyo tangia ilipoanza, michuano hiyo ilishirikisha timu za Tanzania bara, Uganda, Zanzibar na Malawi ambapo kikosi hicho kiliibuka kinara. Mabingwa Zanzibar wamepata kikombe na medali ya dhahabu wakati Malawi wamepata medali ya Fedha, mshindi wa tatu, Tanzania bara ameambulia medali ya shaba Mabingwa wa soka la ufukweni, Zanzibar

MO KUMSHUSHA KOPUNOVIC AKIKABIDHIWA TIMU

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Kuna uhakika mkubwa kuwa aliyekuwa kocha mkuu wa Simba SC, Goran Kopunovic akarejea tena Msimbazi kama kukinoa kikosi hicho kilichotangaza kuachana na kocha wake mkuu Mcameroon, Joseph Omog kufuatia mwenendo mbaya hadi kutolewa mapema katika michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) maarufu kombe la FA. Simba iliondoshwa na timu ya daraja la pili ya Green Warriors ya Mwenge na kuvuliwa ubingwa, Simba ilifungwa mabao 4-3 kwa mikwaju ya penalti baada ya sare ya 1-1 ndani ya dakika 90, baada ya kuondoka Omog, Simba sasa inempa jukumu kocha wake msaidizi Masoud Djuma raia wa Burundi na kocha wa makipa Muharami Mohamed "Shilton". Lakini kuna taarifa njema kuwa mshindi wa zabuni mfanyabiashara, Mohamed Dewji "Mo" ambaye ameshinda zabuni na kununua Hisa asilimia 51za klabu hiyo ana mpango wa kumrejesha kazini kocha Goran Kopunovic ambaye aliwahi kuinoa Simba na kuipa kombe la Mapinduzi, Mo atamrejesha kocha huyo pindi atakapopewa rasm...

Mpiga picha wa Azam Media afariki

Picha
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam Mpiga picha wa televisheni wa kituo cha Azam Tv, Iddy Salum "Mambo" amefariki dunia leo akiwa hospitalini jijini Mwanza alipokuwa akitibiwa. Idd alikuwa maarufu na kamera yake pembeni ya goli wakati kituo hicho kikirekodi mchezo wa Ligi Kuu au nashindano yoyote yanayorushwa na Azam Tv. Mpiga picha huyo mara kwa mara amekuwa akikaa upande wa karibu na vyumba vya kubadilishia jezi wachezaji, mbali na kupiga picha, marehemu pia alikuwa mwandishi wa Azam Media. Mungu amweke mahara pema peponi, Amina Idd Salum 'Mambo' enzi za uhai wake

SIMBA WASEMA HAWATARUDIA MAKOSA KWA NDANDA

Picha
Na  Ikram Khamees. Dar es Salaam Vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara Simba SC, wanaingia kambini leo tayari kujiandaa na mchezo wao wa Ligi Kuu bara dhidi ya Ndanda FC ya mkoani Mtwara utakaofanyika Jumamosi ijayo katika uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara. Simba wanaingia kambini leo kujiandaa na mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya kuvuliwa ubingwa wa michuano ya Azam Sports Fedetation Cup, (ASFC) maarufu kombe la FA na timu ya daraja la pili Green Warriors ya Mwenge kwa mabao 4-3 ya mikwaju ya penalti baada ya sare ya 1-1 ndani ya dakika 90. Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa Simba, Haji Manara amesema hawatakubali kufanya makosa na amesema Ndanda watapata kipigo nyumbani kwao hapo hapo, Simba ipo chini ya kocha msaidizi, Mrundi, Masoud Djuma kufuatia kocha mkuu,Mcameroon Joseph Omog kufutwa kazi kutokana na matokeo mabaya iliyoyapata Simba wataingia kambini leo

TAMBWE ASEMA BADO MBAO FC

Picha
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam Mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Amissi Tambwe amesema baada ya kuwatungua Reha FC katika mchezo wa kombe la Azam Sports Federation Cup, (ASFC) maarufu kombe la FA, amesema bado Mbao FC ambao nao amepanga kuwanyoosha Jumamosi ijayo. Tambwe alikuwa majeruhi kwa muda mrefu lakini juzi alirejea uwanjani na kuiwezesha timu yake ya Yanga kuilaza Reha FC mabao 2-0 uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, timu hizo zilienda kupumzika zikiwa hazijafungana hata bao, lakini kipindi cha pili Yanga walipata mabao hayo mawili yaliyofungwa na Pius Buswita na Tambwe. Kwa Amissi Tambwe hilo lilikuwa bao lake la kwanza msimu huu na pia ulikuwa mchezo wake wa kwanza tangia apone majeraha yake yaliyomweka benchi kwa muda mrefu, katika mazungumzo yake, Tambwe amesema ataendelea kufunga karibu kila mechi na hakuna wa kumzuia

Messi achukua jiko

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Winga wa klabu bingwa ya soka Afrika mashariki na kati, Azam FC, Ramadhan Singano "Messi" ameachana na ukapela baada ya kufanikiwa kufunga ndoa Ijumaa iliyopita. Kwa mujibu wa klabu yake ya Azam FC inapenda kumtakia kheri baada ya kufanya tukio hilo kubwa maishani mwake, Messi aliibukia Simba B mwaka 2013 na alipandishwa kikosi cha wakubwa na kuweza kung' ara. Mchezaji huyo alienda kufanya majaribio katika timu ya Difaa El Jadida ya Morocco ambapo alifaulu lakini alishindwa kujiunga nayo baada ya wakala wake kuigomea timu hiyo iliyotaka kutoa pesa kiduchu juu ya nyota huyo Ramadhan Singano "Messi" akiwa na mkewe baada ya kugunga ndoa yao safi hivi karibuni

KISPOTI

Picha
Simba walikuwa bize na Asante Kwasi wakawasahau Shaaban Dihile na Hussein Bunu. Na Prince Hoza KIUNGO Jonas Gerald Mkude aligongesha mwamba penalti yake na Mohamed Hussein "Tshabalala" akamdakisha kipa wa zamani wa kimataifa nchini Shaaban Dihile, Simba ikitolewa hatua ya 64 bora, sawa na raundi ya pili tu ya kombe la Azam Sports Federation Cup (ASFC) maarufu kombe la FA, Ijumaa iliyopita. Maana yake Simba SC imevuliwa ubingwa wa Azam Sports Federation Cup, baada ya kufungwa kwa penalti 4-3 kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 90 na timu ya Green Warriors ya Mwenge Dar es Salaam inayomilikiwa na Jeshi la Wananchi Tanzania, (JWTZ). Katika mchezo huo uliofanyika uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam kipa wa Simba Aishi Manula alipangua penalti moja ya Zuakuu Mgala kabla ya George Ossey kupiga nje, lakini penalti za Cecil Efraim, Amir Haji, Juma Mdingi na Iddi Nyambi zilimpita. Katika dakika ya 90 za mchezo huo, Green Warriors walitangulia kupata bao dakika ya 43 k...

DK SHEIN AWAJAZA MAMILIONI WACHEZAJI, ZANZIBAR

Picha
Na Mwandishi Wetu. Zanzibar Rais wa serikali ya Baraza la mapinduzi, Zanzibar, Dk Mohames Ally Shein, jana amewazawadia wachezaji wa timu ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes, makocha wake pamoja na viongozi kila mmoja shilingi Milioni 3 za Kitanzania na kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa nyumba, baada ya kuiwezesha Zanzibar kushika nafasi ya pili kombe la Chalenji. Rais Shein amewatunuku mashujaa hao licha ya kufungwa kwa penalti na wenyeji Kenya katika mchezo wa fainali ulioisha kwa sare ya mabao 2-2 ndani ya dakika 120 katika uwanja wa Kemyatta, mjini Machakos nchini Kenya. Zanzibar ilipangwa kundi A pamoja na timu za taifa za Rwanda, Libya, Tanzania bara na Kenya na kuweza kukamata nafasi ya pili ikiwa nyuma ya wenyeji Kenya waliomaliza vinara, katika mchezo wa nusu fainali, Zanzibar iliiondosha Uganda ambao walikuwa mabingwa watetezi. Tangia mwanzo Zanzibar ilionekana kuhimili mikiki mikiki ya michuano ambapo katika mchezo wake wa kwanza iliweza kuilaza Rwanda mabao 3-1 kabla ya ...

DK SHEIN AWAJAZA MAMILIONI WACHEZAJI, ZANZIBAR

Na Mwandishi Wetu. Zanzibar Rais wa serikali ya Baraza la mapinduzi, Zanzibar, Dk Mohames Ally Shein, jana amewazawadia wachezaji wa timu ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes, makocha wake pamoja na viongozi kila mmoja shilingi Milioni 3 za Kitanzania na kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa nyumba, baada ya kuiwezesha Zanzibar kushika nafasi ya pili kombe la Chalenji. Rais Shein amewatunuku mashujaa hao licha ya kufungwa kwa penalti na wenyeji Kenya katika mchezo wa fainali ulioisha kwa sare ya mabao 2-2 ndani ya dakika 120 katika uwanja wa Kemyatta, mjini Machakos nchini Kenya. Zanzibar ilipangwa kundi A pamoja na timu za taifa za Rwanda, Libya, Tanzania bara na Kenya na kuweza kukamata nafasi ya pili ikiwa nyuma ya wenyeji Kenya waliomaliza vinara, katika mchezo wa nusu fainali, Zanzibar iliiondosha Uganda ambao walikuwa mabingwa watetezi. Tangia mwanzo Zanzibar ilionekana kuhimili mikiki mikiki ya michuano ambapo katika mchezo wake wa kwanza iliweza kuilaza Rwanda mabao 3-1 kabla ya ...

TAMBWE AREJEA NA MABAO YAKE, YANGA IKIIFINYANGA REHA FC 2-0

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Klabu bingwa ya soka Tanzania bara, Yanga SC jioni ya leo imefanikiwa kutinga hatua ya 32 bora ya kombe la Azam Sports Federation Cup (ASFC) maarufu kombe la FA baada ya kuilaza Reha FC ya Chang' ombe mabao 2-0 uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Vijana wa Reha waliidhibiti Yanga hadi mapumziko wakienda sare tasa 0-0, kipindi cha pili Reha FC nao walilitia msukosuko lango la Yanga na kuambulia kupata kona mbili mfululizo ambazo hazikuzaa matunda. Kocha msaidizi wa Yanga shadrack Nsajigwa "Fuso" alijaribu kubadili kikosi angalau kupata bao la kuongoza na la ushindi. Yanga waliamka dakika za mwishoni na kujipatia mabao yake mawili kupitia kwa Pius Buswita na Amissi Tambwe ambao ni mchezo wake wa kwanza tangu arejee uwanjani. Juzi watani zao Simba SC ilivuliwa ubingwa wa michuano hiyo baada ya kufungwa na timu ya daraja la pili ya Green Warriors mabao 4-3 kufuatia sare ya bao 1-1 ndani ya dakika ya 90 Amissi Tambwe amerejea kwa kasi ...

YANGA NAO USO KWA USO NA KITIMU CHA DARAJA LA PILI

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Mabingwa wa soka Tanzania bara, Yanga SC, jioni ya leo inatelemka uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kucheza na timu ya Daraja la pili ya Reha FC yenye maskani yake Chang' ombe Dar es Salaam mchezo wa raundi ya 64 bora michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) maarufy kombe la FA. Yanga ikiwa na furaha ya kurejea kwa mastaa wake waliokuwa majeruhi, itangia uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya watani zao Simba ambao juzi waliondolewa katika michuano hiyo na kuvuliwa ubingwa wao na kitimu cha Daraja la pili cha Green Warriors. Hivyo nao watauchukulia mchezo huo kuwa ni mkubwa kwao kwani watani zao Simba wamemfurusha kocha wao baada ya kipigo hicho, Yanga walivuliwa ubingwa na Mbao FC katika hatua ya robo fainali Yanga SC jioni ya leo wataimana na Reha FC

NDANDA KUCHELE WAIENDEA SIMBA MAFICHONI, WADAI WANATAKA KUTONESHA KIDONDA

Picha
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam Timu ya Ndanda FC maarufu Wana kuchele, wameingia mafichoni kwenye fukwe za bahari ikiwa tayari kwa kutonesha kidonda cha Wana Msimbazi ambapo watakutana nao mwishoni mwa wiki ijayo. Kikosi hicho kilichoongezewa na Mrisho Ngasa "Anko", Salum Telela na Ame Ally "Zungu" waliosajiliwa dirisha dogo, wameahidi kuishinda Simba katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara utakaopigwa uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara. Kikosi hicho kimejificha pembezoni mwa bahari kikiweka kambi kwenye hoteli moja ambapo viongozi wa timu hiyo wanafanya siri ili Simba wasije kujua wanachotaka kuwafanya, hata hivyo Ndanda wamesema lengo lao ni kutonesha kidonda cha Simba aliyejeruhiwa na maaskari wa JWTZ, Green Warriors Ndanda FC wakijifua vikali kuingoja Simba

Azam FC hakuna kuremba, yaifumua Arie C 4-0

Picha
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam Klabu bingwa Afrika mashariki na kati, Azam FC usiku huu imetinga hatua ya 32 bora ya mashindano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) maarufu kombe la FA baada ya kuifumua bila huruma timu ya Arie C mabao 4-0 uwanja wa Azam Complex , Chamazi. Mabingwa hao wa Afrika mashariki na kati maarufu kombe la Kagame wanaonolewa na Mromania, Aristica Cioaba, waliutawala mchezo huo karibu vipindi vyote viwili, hadi mapumziko Azam walikuwa wakiongoza kwa mabao matatu. Mabao ya Azam yamefungwa na Salmin Hoza dakika ya 17, Agrey Morris dakika ya 34 na Yahya Zayd dakika ya 41 aliyeunganisha mpira wa kona uliopigwa na Mghana Enock Atta. Enock Atta naye aliiandikia Azam bao la nne kipindi cha pili dakika ya 53 akiunganisha krosi ya Mzimbabwe Bruce Kangwa, kesho mabingwa wa Tanzania bara Yanga SC watacheza na Reha FC uwanja wa Uhuru Dar es Salaam Azam FC usiku huu imeifunga Arie C mabao 4-0

Azam FC hakuna kuremba, yaifumua Arie C 4-0

Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam Klabu bingwa Afrika mashariki na kati, Azam FC usiku huu imetinga hatua ya 32 bora ya mashindano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) maarufu kombe la FA baada ya kuifumua bila huruma timu ya Arie C mabao 4-0 uwanja wa Azam Complex , Chamazi. Mabingwa hao wa Afrika mashariki na kati maarufu kombe la Kagame wanaonolewa na Mromania, Aristica Cioaba, waliutawala mchezo huo karibu vipindi vyote viwili, hadi mapumziko Azam walikuwa wakiongoza kwa mabao matatu. Mabao ya Azam yamefungwa na Salmin Hoza dakika ya 17, Agrey Morris dakika ya 34 na Yahya Zayd dakika ya 41 aliyeunganisha mpira wa kona uliopigwa na Mghana Enock Atta. Enock Atta naye aliiandikia Azam bao la nne kipindi cha pili dakika ya 53 akiunganisha krosi ya Mzimbabwe Bruce Kangwa, kesho mabingwa wa Tanzania bara Yanga SC watacheza na Reha FC uwanja wa Uhuru Dar es Salaam

Simba waachana na Omog, kisa Green Warriors

Picha
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam Baada ya kuvuliwa ubingwa wa kombe la FA jana na vijana wa Green Warriors ya Mwenge kwa mikwaju ya penalti 4-3 uwanja wa Azam Complex, Uongozi wa Simba SC, imevunja mkataba na kocha wake mkuu, Mcameroon, Joseph Marius Omog. Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa klabu ya Simba, Haji Manara amethibitisha kuvunjwa kwa mkataba huo na sasa timu itakuwa chini ya msaidizi wake Mrundi, Masoud Djuma. Manara amesema kufungwa kwa Simba na vijana wa Green Warriors kwa mikwaju ya penalti baada ya kumaliza dakika 90 kwa kufungana 1-1. Mashabiki wa Simba hawakuridhishwa na matokeo hayo na walitaka kocha huyo afutwe kazi kwakuwa Green Warriors hawakustahili kufika kwenye hatua ya matuta, Omog ameiwezesha Simba kufika kombe la Shirikisho barani Afrika mwakani na pia inakamata kiti cha uongozi wa Ligi Kuu bara Kocha Mcameroon Joseph Omog aliyesimama amefutwa kazi

JKT Ruvu yabadili jina

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Baada ya Shirikisho la soka nchini, (TFF) kuwataka wamiliki wa timu kuhakikisha timu zao hizo hazishiriki ligi moja na ikitokea hivyo basi moja wapo inaenguliwa, tayari Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limeanza kuachana na timu zake na kubakiwa na moja tu ambayo itashiriki Ligi Kuu ama Ligi Daraja la kwanza. Jeshi hilo limetoa msimamo wake ambapo sasa timu ya JKT Ruvu iliyokuwa na maskani yake Mlandizi mkoani Pwani, na kuhamia Mlalakua Dar es Salaam, sasa timu hiyo imebadili jina na inaitwa JKT Tanzania FC, mmoja wa wasemaji wa jeshi hilo amesema kuwa nchi nzima timu inayomilikiwa na jeshi hilo ni hiyo tu. Timu za Ruvu Shooting, JKT Mgambo, JKT Orjolo, JKT Kanemba, JKT Mlale na nyinginezo sasa zitasimamiwa na wananchi wa maeneo husika na si JKT tena kama ilivyozoeleka JKT Ruvu sasa inaitwa JKT Tanzania FC

Yanga yachomoza CAF kwa ubora wa kandanda Afrika

Picha
Na Saida Salum. Dar es Salaam Shirikisho la kandanda barani Afrika, CAF, limetaja viwango vipya vya ubora wa kandanda kwa vilabu huku timu ya Esperance ya Tunisia ikiongoza, katika toleo lao lililochapishwa hivi karibuni limeziweka pia klabu tatu za Tanzania ambazo ni Yanga, Azam na Simba. Yanga SC ambao mwakani watashiriki michuano ya Caf ikicheza Ligi ya mabingwa, inaongoza katika viwango hivyo kwa upande wa timu za Tanzania ikishikilia nafasi ya 345 ikifuatiwa na Azam FC iliyo katika nafasi ya 365. Wekundu wa Msimbazi ambao na mwakani watashiriki michuano inayoandaliwa na Caf ya kombe la Shirikisho, yenyewe inakamata nafasi ya 371, hata hivyo Simba haikupata nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa kwa kipindi cha miaka minne jambo ambalo limepelekea timu hiyo iliyowahi kuingia fainali ya kombe la Caf mwaka 1993 kushuka Yanga imetajwa kushika nafasi ya 345 kwa ubora wa kandanda Afrika

SIMBA YAVULIWA UBINGWA WA FA, YAPIGWA NA KITIMU CHA DARAJA LA PILI

Picha
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam Mabingwa watetezi wa kombe la Azam Sports Federation Cup (ASFC) maarufu kombe la FA, Simba SC usiku huu wamevuliwa ubingwa na timu ya daraja la pili ya Green Worriors kwa mabao 4-3 kwa mikwaju ya penalti kufuatia sare ya bao 1-1 ndani ya dakika 90. Mchezo wa ufunguzi kwa mabingwa hao watetezi uliofanyika uwanja wa Azam Complex, Chamazi, na vijana wa Green Worriors kulitia msukosuko lango la Simba mara kwa mara, Hussein Bunu alitangulia kuifungia Worriors bao la kuongoza kipindi cha kwanza, kabla ya John Bocco "Adebayor" kuisawazishia Simba kwa penalti. Hadi mpira unamalizika timu hizo zilikuwa sare 1-1, na ndipo zilipoelekea katika mikwaju ya penalti ambapo Simba imetupwa nje huku vijana wa Green Worriors wakitinga hatua ya 32 bora, kesho uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, Yanga SC watacheza na Reha FC Simba SC imevuliwa ubingwa wa FA leo

Mkuu wa mkoa Dar es Salaam, apewa shavu Yanga

Picha
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam Aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Said Meki Sadiki ameteuliwa kuwa mjumbe kwenye kamati mpya iliyoundwa kuelekea katika mfumo wa mabadiliko utakaoifanya klabu hiyo kuwa kampuni ya kuuza Hisa kama ilivyo kwa watani zao Simba SC. Mwanasheria Alex Gaitani Mgongolwa amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa kamati hiyo iliyowahusisha wataalamu wa sheria na uchumi, Profesa Mgongo Fimbo naye amechaguliwa kuwa mjumbe wa upande wa masuala ya katiba wakati Mohamed Nyenge anakuwa mjumbe masuala ya uchumi na fedha, George Fumbuka, Masuala ya uwekezaji na mshauri wakati Felix Mlaki, uchumi na fedha. Meki Sadiki mbali na kuongoza mkoa wa Dar es Salaam wakati wa utawala wa awamu ya nne ya Jakaya Kikwete, akaongoza pia mkoa wa Kilimanjaro katika utawala wa awamu ya tano ya John Pombe Magufuli kabla ya kustaafu. Klabu ya Yanga inatarajia rasmi kuingia kwenye soko la Hisa na kuna uwezekano mkubwa timu hiyo ikaangukia kwa bilionea ambaye atanunua Hisa asilimia 49 na asili...

Lipuli yanyoosha mikono kwa Asante Kwasi

Picha
Na Saida Salum. Dar es Salaam Uongozi wa timu ya Lipuli FC "Wanapaluhengo" umemnyooshea mikono mlinzi wake Asante Kwasi raia wa Ghana kujiunga na vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara, Simba SC baada ya mvutano mrefu uliodumu karibu majuma mawili kuhusu usajili wake. Akizungumza leo, mwenyekiti wa Lipuli FC, Ramadhan Mahano amesema umefika mwisho sasa wa kulumbana kuhusu mchezaji Asante Kwasi kwakuwa tayari uongozi wa Simba ulishawafuata na kumuhitaji mchezaji huyo hivyo nao wameona ni bora kuwaachia Simba. Mahano amesema kuwa Kwasi alikuwa mchezaji halali wa Lipuli waliyemsajili mwanzoni mwa msimu huu kwa mkataba wa mwaka mmoja akitokea Mbao FC ya Mwanza na Simba imekubali kulipa ada ya kumnunua mchezaji huyo ingawa hakuweka wazi ni kiasi gani kitatolewa na Simba. Mambo Uwanjani inafahamu kuwa Simba itatoa shilingi Milioni 25 kama ada ya usajili kwa mchezaji huyo, Kwasi ataanza kuitumikia Simba kwenye hatua onayofuata ya Ligi Kuu bara na michuano ya kombe la Mapind...

Kagera Sugar yatuma salamu kombe la FA

Picha
Na Paskal Beatus. Bukoba Timu ya Kagera Sugar ya Bukoba jana ilifanikiwa kuingia hatua ya 32 bora ya michuano ya Azam Sports Federation Cup, maarufu kombe la FA baada ya kuichakaza timu ya Makambako mabao 7-0 uwanja wa Kaitaba, Bukoba. Mshambuliaji wake mkongwe Themi Felix "Mnyama" aligeuka shujaa baada ya kufunga magoli matatu peke yake (Hat trick) huku Peter Mwalyanzi akifanikiwa kufunga magoli mawili na Venance Ludovic na Mwahita Salehe wakifunga goli moja kila mmoja. Kwa ushindi huo mkubwa kabisa ilioupata Kagera Sugar ni kama salamu kwa mabingwa watetezi Simba SC ambao leo wanashuka uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam kuanza kutetea taji lake huku wakiwaza makali ya Kagera Sugar Themi Felix (Kulia) amefunga magoli matatu jana

STAA WETU

Picha
Simon Msuva: Mtanzania mwenye njaa ya mafanikio. Na Prince Hoza JICHO la kila Mtanzania lilikuwa kwa Mbwana Ally Samata anayeichezea timu ya Ligi Kuu Ubelgiji ya KRC Genk, Samata ni Mtanzania na mzaliwa wa Mbagala jijini Dar es Salaam ambaye amecheza Kimbangulile Academy, Mbagala Market (African Lyon), Simba SC na TP Mazembe ya DR Congo. Samata amepata heshima kubwa kwenye mchezo wa soka na kuiweka pazuri Tanzania akisaidia kuitangaza, Samata amekuwa balozi mzuri akiwa na TP Mazembe ambapo amefanikiwa kubeba taji la Afrika na kuweza kushinda tuzo ya mwanasoka bora Afrika kwa mchezaji anayecheza ligi ya nyumbani, hakuna Mtanzania mwingine aliyewahi kushinda tuzo hiyo. Baada ya mafanikio hayo, timu za Ulaya zikaanza kumtolea macho, na kwa bahati nzuri KRC Genk ikafanikiwa kumchukua na sasa ni mchezaji wa timu hiyo, tayari nyota yake inang' ara, akiisaidia timu hiyo kufanya vizuri kwenye Ligi ya Ubelgiji, na ubora wake ukapelekea kukamiwa mno na mabeki wa timu pinzani. Na sasa Sa...

CHALENJI YAIPOROMOSHA TANZANIA VIWANGO FIFA

Picha
Mrisho Hassan. Dar es Salaam Baada ya kuvurunda katika michuano ya kombe la Chalenji, Tanzania imeporomoka kwa nafasi tano zaidi kwa mwezi Desemba katika viwango vya ubora wa kutandaza kandanda ulimwenguni vinavyotolewa kila mwezi na Shirikisho la mpira wa miguu duniani, (FIFA). Katika viwango vilivyotolewa na Shirikisho hilo na kutangazwa leo, Tanzania imeshuka kutoka nafasi ya 142 hadi 147 huku Uganda ikiendelea kuongoza katika ukanda wa Afrika mashariki na vilevile kukamata nafasi ya 75 kwa Afrika. Kuporomoka kwa Tanzania kumechangiwa zaidi na matokeo mabovu iliyoyapata katika michuano ya mataifa Afrika mashariki na kati, maarufu Chalenji yaliyomalizika juma lililopita na Kenya kutwaa ubingwa kwa kuifunga Zanzibar kwa mikwaju ya penalti 3-2 kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 120 Tanzania imeporomoka tena FIFA

SIMBA YAACHANA NA STRAIKA WA MSUMBIJI NA ZAMBIA

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Uongozi wa klabu ya Simba ya Dar es Salaam umesitisha mpango wa kuwasajili washambuliaji Antonio Dayo Domingues wa Ferreviaro De Beira ya Msumbiji na Jonas Sekuhawa kutoka Zambia. Mwenyekiti wa kamati ya usajili Zachatia Hanspoppe amesema wameamua kusitisha mpango huo na sasa watamsajili mchezaji mmoja tu wa kigeni ambaye ni Asante Kwasi kutoka Lipuli ya Iringa. Aidha Hanspoppe ambaye ni kapteni mstaafu wa Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ), amesema wachezaji Laudit Mavugo na Nicolaus Gyan hawataachwa isipokuwa Method Mwanjale ndiye aliyeachwa Simba imeachana na Domingues na Sekuhawa

SIMBA MGUU SAWA KUTETEA FA KWA GREEN WORRIORS, KESHO

Picha
Na Saida Salum. Dar es Salaam Kikosi cha Simba jana jioni kiliendelea na mazoezi yake chini ya Kocha Joseph Omog akisaidiana na kocha msaidizi Massoud Djuma. Akielezea maandalizi ya mchezo maalumu wa ufunguzi wa michuano ya Azam Federetion Cup kocha Omog alisema 'Tunajiandaa vyema kutetea kombe hili, siku ya Ijumaa tutakuwa na mchezo wetu wa kwanza kwenye michuano hii msimu huu dhidi ya Green Warriors na tunaendelea kujiandaa vyema. Mashabiki waje kwa wingi siku hiyo kwa ajili ya kutupa sapoti ambayo wamekuwa wakitupa kila mahali kikosi chetu kinapokwenda na sisi tunaimani ya kufanya vizuri kwani tumejiandaa vizuri' Kocha Omog amerejea nchini Tarehe 14.12.2017 ambapo alikwenda nchini Cameroon kwenye mapumziko mafupi. Simba wataikabili Green Worriors kesho

Yanga yaipashia Reha FC kombe la FA

Picha
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam Mabingwa wa soka nchini, Yanga SC jana wameendelea kujifua kwa ajili ya mchezo wao wa michuano ya Azam Sports Federation Cup, maarufu kombe la FA ambapo Jumapili ijayo itacheza na timu ya Reha FC inayoshiriki Ligi daraja la pili (SDL). Katibu mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa amesema kikosi chake kipo tayari kwa mchezo huo na kinachompa jeuri ni kurejea uwanjani kwa wachezaji wake ambao walikosekana muda mrefu kutokana na majeruhi, Amissi Tambwe ni miongoni mwa wachezaji majeruhi wa muda mrefu ambapo sasa ataanza kucheza kwenye ahindano hilo la FA. Pia nyota wengine kama Donald Ngoma, Thabani Kamusoko na Papy Kabamba Tshishimbi nao ni miongoni mwa wachezaji walioanza kuitumikia timu hiyo na huenda katika mchezo wao wa Ligi Kuu bara dhidi ya Mbao FC wakaanza Yanga watacheza na Reha FC kombe la FA

Milambo FC yatupwa nje kombe la FA

Picha
Na Emil Kasapa. Tabora Timu ya Milambo Fc ya Tabora imeondolewa katika hatua ya pili ya michuano ya kombe la shirikisho nchini baada kufungwa kwa penati 3-1 na timu ya Buseresere ya GEITA mara baada ya sare ya bao mbili kwa mbili ndani ya dakika 90. Salum Moshi alikuwa wa kwanza kuifungia Buseresere dk ya  19 kabla ya Shaban Madanganya kusawazisha dk ya 44. Kipindi cha pili Abuu wakati alijifunga dk 67 kabla ya Peter Croach kusawazisha dk ya 75. Milambo walipata penati kupitia kwa Yohana John wakati Lucas Misana,Rashid Kopa na Fidelai Philimon wote walikosa Kwa upande wa Buseresere walipata kupitia kwa Aman Abud ,Nicholous Samwery na Kassim Ibrahim wakati Juma Nade na Lameck Masabo walikosa mikwaju yao ya penati. Kesho katika uwanja wa Mwinyi Rhino watacheza na Alliance ya mwanza katika mwendelezo wa mashindano hayo. Milambo imetupwa nje kombe la FA

Dili la Asante Kwasi laiva Simba, Hanspoppe aanika kila kitu

Picha
Na Saida Salum. Dar es Salaam Baada ya mvutano wa muda mrefu baina ya viongozi wa vilabu vya Simba ya Dar es Salaam na Lipuli ya Iringa, juu ya mchezaji Asante Kwasi raia wa Ghana, sasa mambo yameanza kuwa mazuri kufuatia mwenyekiti wa kamati ya usajili wa Simba, Zacharia Hanspope kuanika ukweli. Akizungumza jioni ya leo, Hanspoppe amedai mipango ya kumnasa beki huyo mwenye mabao matano Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara imeenda vizuri na huenda akaitumikia klabu yake mpya ya Wekundu wa Msimbazi katika michuano ya kombe la Mapinduzi, FA na Ligi Kuu bara. Tayari beki huyo ameshasaini Simba ingawa bado ana mkataba na Lipuli, lakini viongozi wa Lipuli wameilalamikia Simba kwa kushindwa kuwasiliana na Lipuli na kuvunja sheria kwa kumsainisha kinguvu, kwa mujibu wa Hanspope, Simba imetuma maombi ya kumuhitaji mlinzi huyo wa kimataifa Asante Kwasi anakaribia kujiunga na Simba

MEXIME ATAMBIA ATUPELE, ATHANAS

Picha
Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam Kocha mkuu wa timu ya soka ya Kagera Sugar ya Misenyi Bukoba mkoani Kagera, Mecky Mexime ameonyesha kufurahishwa na safu yake mpya ya ushambuliaji kufuatia usajili uliofanywa na kikosi chake kwa Atupele Green na Pastory Athanas. Akizungumza hivi karibuni mara baada ya usajili huo, Mexime amesema ana imani na ujio wa mshambuliaji Atupele Green na winga Pastory Athanas utawapa jeuri ya kufanya vizuri katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara na michuano ya kombe la FA. Kocha huyo amedai, anawafahamu vema wachezaji hao ni wazuri na wataweza kuisaidia timu kuweza kupambana vikali kwenye ligi hiyo na huenda wakarejea kwenye nafasi za juu kama ilivyokuwa kwa msimu uliopita. Atupele na Athanas wote kwa pamoja wameachwa na Singida United, Atupele amewahi kucheza Kagera Sugar, Coastal Union, Ndanda na Yanga, wakati Athanas amecheza Stand United, Simba SC na Singida United Mecky Mexime anajivunja uwepo wa Atupele Green na Pastory Athanas

NJOMBE MJI YANASA WANYARWANDA WAWILI, MSIMU HUU KAZI IPO

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Timu ya Njombe Mji FC ya mkoani Njombe ambayo inashiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara, imefanikiwa kuwasainisha nyota wawili wa kimataifa kutoka nchini Rwanda ambao wataungana na nyota wengine watatu wa hapa nchini waliosajiliwa katika dirisha dogo linalotarajia kufungwa Desemba 23. Akizungumza na Mambo Uwanjani, Afisa Habari wa Njombe Mji, Solanus Mhagama amewataja wachezaji hao ni Herelimana Lewi kutoka Mukura Victory na Etienne Ngladjo wa Sunrise FC zote za Rwanda. Aidha Mhagama amewataja Muhsin Malima na Nelson Kibabage wa Mtibwa Sugar nao wamejiunga na timu hiyo kwa mkopo huku pia wakimnasa Mohamed Titi kutoka Singida United, kwa usajili huo Njombe Mji inaweza kutoa ushindani mkubwa na kuweza kujikongoja kutoka nafasi za mkiani, timu hiyo inashika nafasi ya 15 ikiwa ya pili kutoka ya mwisho na imecheza mechi 11 Njombe Mji FC imeiongeza wachezaji watano dirisha dogo

AZAM FC YAWALAMBISHA ICE CREAM, POLISI TANZANIA

Picha
Na Paskal Beatus. Dar es Salaam Mabingwa wa soka wa kombe la Kagame, Azam FC usiku huu imeifunga bila huruma timu ya maafande wa Jeshi la Polisi Tanzania kwa mabao 3-1 mchezo wa kirafiki uliofanyika uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. Polisi Tanzania ambayo Jumapili iliyopita iliilazimisha sare tasa 0-0 mabingwa wa soka nchini Yanga, leo wameshindwa kufurukuta mbele ya wauza Ice cream hao wa Bakhresa, Polisi walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa kipindi cha kwanza na kwenda mapumziko wakiwa mbele. Kocha wa Azam alifanya mabadiliko kipindi cha pili kwa kuwaingiza Peter Paul na Waziri Junior, mabadiliko yaliyozaa matunda kwani Paul alifunga mawili na Junior akafunga lingine moja la ushindi, huo ni ushindi wa tatu mfululizo kwa Azam baada ya kuifunga Mvuvumwa 8-1, Villa Squad 7-1 na leo 3-1 dhidi ya Polisi Tanzania Azam FC imefunga Polisi Tanzania jana

Mapokezi Zanzibar Heroes yatikisa

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Wananchi wanaotoka miji mbalimbali visiwani Zanzibar jana wameipokea timu yao ya taifa, Zanzibar Heroes iliyorejea ikitokea katika mji wa Machakos nchini Kenya ambako ilienda kushiriki michuano ya mataifa Afrika mashariki na kati, maarufu kombe la Chalenji. Zanzibar ilidanikiwa kuingia fainali ambapo juzi ilichuana vikali na mwenyeji Kenya, Harambee Stars na katika mchezo huo Kenya ilishinda mabao 3-2 kwa mikwaju ya penalti kufuatia kumaliza dakika 120 kwa sare ya 2-2, mashujaa hao walipokewa kifalme ambapo maelfu ya Wazanzibar walijipanga kando kando ya barabara kuilaki timu hiyo. Zanzibar imefanikiwa kuingia hatua hiyo ya fainali kwa mara ya pili, mwaka 1995 Zanzibar ilifanikiwa kuingia fainali ya michuano hiyo ya Chalenji ilipofanyika nchini Uganda na ikafanikiwa kutwaa ubingwa, lakini majuzi ilishindwa kurudia historia yake iliyoiweka Wachezaji wa Zanzibar Heroes wakiwapungia mikono wananchi waliojitokeza kuwalaki jana Wananchi wamejipanga ba...