Dili la Asante Kwasi laiva Simba, Hanspoppe aanika kila kitu

Na Saida Salum. Dar es Salaam

Baada ya mvutano wa muda mrefu baina ya viongozi wa vilabu vya Simba ya Dar es Salaam na Lipuli ya Iringa, juu ya mchezaji Asante Kwasi raia wa Ghana, sasa mambo yameanza kuwa mazuri kufuatia mwenyekiti wa kamati ya usajili wa Simba, Zacharia Hanspope kuanika ukweli.

Akizungumza jioni ya leo, Hanspoppe amedai mipango ya kumnasa beki huyo mwenye mabao matano Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara imeenda vizuri na huenda akaitumikia klabu yake mpya ya Wekundu wa Msimbazi katika michuano ya kombe la Mapinduzi, FA na Ligi Kuu bara.

Tayari beki huyo ameshasaini Simba ingawa bado ana mkataba na Lipuli, lakini viongozi wa Lipuli wameilalamikia Simba kwa kushindwa kuwasiliana na Lipuli na kuvunja sheria kwa kumsainisha kinguvu, kwa mujibu wa Hanspope, Simba imetuma maombi ya kumuhitaji mlinzi huyo wa kimataifa

Asante Kwasi anakaribia kujiunga na Simba

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA