NJOMBE MJI YANASA WANYARWANDA WAWILI, MSIMU HUU KAZI IPO

Na Ikram Khamees. Dar es Salaam

Timu ya Njombe Mji FC ya mkoani Njombe ambayo inashiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara, imefanikiwa kuwasainisha nyota wawili wa kimataifa kutoka nchini Rwanda ambao wataungana na nyota wengine watatu wa hapa nchini waliosajiliwa katika dirisha dogo linalotarajia kufungwa Desemba 23.

Akizungumza na Mambo Uwanjani, Afisa Habari wa Njombe Mji, Solanus Mhagama amewataja wachezaji hao ni Herelimana Lewi kutoka Mukura Victory na Etienne Ngladjo wa Sunrise FC zote za Rwanda.

Aidha Mhagama amewataja Muhsin Malima na Nelson Kibabage wa Mtibwa Sugar nao wamejiunga na timu hiyo kwa mkopo huku pia wakimnasa Mohamed Titi kutoka Singida United, kwa usajili huo Njombe Mji inaweza kutoa ushindani mkubwa na kuweza kujikongoja kutoka nafasi za mkiani, timu hiyo inashika nafasi ya 15 ikiwa ya pili kutoka ya mwisho na imecheza mechi 11

Njombe Mji FC imeiongeza wachezaji watano dirisha dogo

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA