Mapokezi Zanzibar Heroes yatikisa

Na Ikram Khamees. Dar es Salaam

Wananchi wanaotoka miji mbalimbali visiwani Zanzibar jana wameipokea timu yao ya taifa, Zanzibar Heroes iliyorejea ikitokea katika mji wa Machakos nchini Kenya ambako ilienda kushiriki michuano ya mataifa Afrika mashariki na kati, maarufu kombe la Chalenji.

Zanzibar ilidanikiwa kuingia fainali ambapo juzi ilichuana vikali na mwenyeji Kenya, Harambee Stars na katika mchezo huo Kenya ilishinda mabao 3-2 kwa mikwaju ya penalti kufuatia kumaliza dakika 120 kwa sare ya 2-2, mashujaa hao walipokewa kifalme ambapo maelfu ya Wazanzibar walijipanga kando kando ya barabara kuilaki timu hiyo.

Zanzibar imefanikiwa kuingia hatua hiyo ya fainali kwa mara ya pili, mwaka 1995 Zanzibar ilifanikiwa kuingia fainali ya michuano hiyo ya Chalenji ilipofanyika nchini Uganda na ikafanikiwa kutwaa ubingwa, lakini majuzi ilishindwa kurudia historia yake iliyoiweka

Wachezaji wa Zanzibar Heroes wakiwapungia mikono wananchi waliojitokeza kuwalaki jana
Wananchi wamejipanga barabarani kuwapokea mashujaa wao wa Zanzibar Heroes jana
Wananchi wengi walifurika kuitazama timu yao iliyoitoa kimasomaso Zanzibar

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA