Kagera Sugar yatuma salamu kombe la FA
Na Paskal Beatus. Bukoba
Timu ya Kagera Sugar ya Bukoba jana ilifanikiwa kuingia hatua ya 32 bora ya michuano ya Azam Sports Federation Cup, maarufu kombe la FA baada ya kuichakaza timu ya Makambako mabao 7-0 uwanja wa Kaitaba, Bukoba.
Mshambuliaji wake mkongwe Themi Felix "Mnyama" aligeuka shujaa baada ya kufunga magoli matatu peke yake (Hat trick) huku Peter Mwalyanzi akifanikiwa kufunga magoli mawili na Venance Ludovic na Mwahita Salehe wakifunga goli moja kila mmoja.
Kwa ushindi huo mkubwa kabisa ilioupata Kagera Sugar ni kama salamu kwa mabingwa watetezi Simba SC ambao leo wanashuka uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam kuanza kutetea taji lake huku wakiwaza makali ya Kagera Sugar