LEONARDA AFUNIKA VIDEO YA HAMOSNOTA
Na Saida Salum. Dar es Salaam
Video queen anayechipukia katika kiwanda cha muziki bongo, Leonarda Wolper ameweza kuwa kivutio kwenye video ya msanii wa bongofleva, Hamosnota.
Watu waliotazama video hiyo wamesema mwanadada huyo ametokelezea vizuri kuliko hata video queen wa wimbo huo, Leonarda ameuza sura mara moja katika wimbo wa Pole wa msanii huyo lakini amefunika mno.
Leonarda pia ni muigizaji na anatarajia kuonekana katika filamu mpya inayotarajia kutoka ya msanii Elia Daniel, mbali na kushiriki katika video ya Hamosnota, Leonarda ameonekana pia kwenye wimbo wa Lava Lava