Simba waachana na Omog, kisa Green Warriors
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam
Baada ya kuvuliwa ubingwa wa kombe la FA jana na vijana wa Green Warriors ya Mwenge kwa mikwaju ya penalti 4-3 uwanja wa Azam Complex, Uongozi wa Simba SC, imevunja mkataba na kocha wake mkuu, Mcameroon, Joseph Marius Omog.
Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa klabu ya Simba, Haji Manara amethibitisha kuvunjwa kwa mkataba huo na sasa timu itakuwa chini ya msaidizi wake Mrundi, Masoud Djuma.
Manara amesema kufungwa kwa Simba na vijana wa Green Warriors kwa mikwaju ya penalti baada ya kumaliza dakika 90 kwa kufungana 1-1.
Mashabiki wa Simba hawakuridhishwa na matokeo hayo na walitaka kocha huyo afutwe kazi kwakuwa Green Warriors hawakustahili kufika kwenye hatua ya matuta, Omog ameiwezesha Simba kufika kombe la Shirikisho barani Afrika mwakani na pia inakamata kiti cha uongozi wa Ligi Kuu bara