Mourinho amkataa Griezmann, Barcelona wachekelea
Manchester United Hawana Mpango tena wa kutaka kumuongeza Mfaransa Antoine Griezmann baada ya kocha Mwenye Maneno Mengi Mreno Josee Mourinho kudai hajaridhishwa na kiasi anachouzwa nyota huyo anaekipiga kunako Klabu ya Atletico Madrid ya Spain.
Taarifa kutoka Gazeti la Marca zinasema Mourinho hajashawishika na kiwango kikubwa cha Fedha anachouzwa Mfaransa huyo ili aweze kutua kwenye Premier League na kusisitiza hata msimu uliopita Board ndio ilikuwa imeshawishika zaidi kutaka kumsajili.
Baada ya mwaka kumalizika Atletico Madrid watakuwa wamemaliza adhabu yao ya kutokusajili na Tayari watakuwa na Mshambuliaji wao kwa Mara nyingine Diego Costa (Burrega)Kitendo kinachoonyesha kuwa Griezmann ataondoka ndani ya klabu kitendo kitakachofungua Milango kwa Barcelona kuona namna ya kumpata Antoine Griezmann ambae anapatikana kwa kitika cha €100 Million (£88).
Hata hivyo Barcelona wanabaki njia panda kuhusu nani asajiliwe Kati ya Antoine Griezmann au Mbrazili Phillipe Coutinho baada ya kuendelea kuonyesha nia ya dhati ya kumuhitaji Coutinho ambae walimkosa msimu uliopita licha ya kupeleka Offer tatu katika Nyakati Tofauti kwa ofa ya £100m.