Messi achukua jiko
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Winga wa klabu bingwa ya soka Afrika mashariki na kati, Azam FC, Ramadhan Singano "Messi" ameachana na ukapela baada ya kufanikiwa kufunga ndoa Ijumaa iliyopita.
Kwa mujibu wa klabu yake ya Azam FC inapenda kumtakia kheri baada ya kufanya tukio hilo kubwa maishani mwake, Messi aliibukia Simba B mwaka 2013 na alipandishwa kikosi cha wakubwa na kuweza kung' ara.
Mchezaji huyo alienda kufanya majaribio katika timu ya Difaa El Jadida ya Morocco ambapo alifaulu lakini alishindwa kujiunga nayo baada ya wakala wake kuigomea timu hiyo iliyotaka kutoa pesa kiduchu juu ya nyota huyo