Mwinyi Haji kutimkia AFC Leopards

Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam

Mlinzi wa kushoto wa mabingwa wa soka nchini, Yanga SC, Mwinyi Haji Mngwali ameuandikia barua uongozi wa Yanga akitaka imwachilie akajiunge na AFC Leopards ya Kenya baada ya kuchoka kukalia benchi, Mwinyi alitamba katika michuano ya kombe la Chalenji iliyofanyika hivi karibuni nchini Kenya.

Mwinyi alikuwa na kikosi cha timu ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes ambacho kilimaliza katika nafasi ya pili, beki huyo amekuwa apewi nafasi ya kucheza katika kikosi cha Yanga na Gerdiel Michael aliyesajiliwa kutoka Azam FC msimu huu ndiye amekuwa akianza katika kikosi cha kwanza cha mabingwa hao wa Bara.

Lakini kwa uwezo mkubwa aliouonyesha Mwinyi katika michuano ya Chalenji na kuivutia timu ya AFC Leopards inayoshiriki Ligi Kuu ya Kenya (KPL) ambapo imetangaza kumsajili, hivyo beki huyo ameandika barua kwa waajiri wake waweze kumwachilia akajiunge na timu hiyo.

Mwinyo Haji Mngwali anataka kuondoka Yanga

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA