NDANDA KUCHELE WAIENDEA SIMBA MAFICHONI, WADAI WANATAKA KUTONESHA KIDONDA
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam
Timu ya Ndanda FC maarufu Wana kuchele, wameingia mafichoni kwenye fukwe za bahari ikiwa tayari kwa kutonesha kidonda cha Wana Msimbazi ambapo watakutana nao mwishoni mwa wiki ijayo.
Kikosi hicho kilichoongezewa na Mrisho Ngasa "Anko", Salum Telela na Ame Ally "Zungu" waliosajiliwa dirisha dogo, wameahidi kuishinda Simba katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara utakaopigwa uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
Kikosi hicho kimejificha pembezoni mwa bahari kikiweka kambi kwenye hoteli moja ambapo viongozi wa timu hiyo wanafanya siri ili Simba wasije kujua wanachotaka kuwafanya, hata hivyo Ndanda wamesema lengo lao ni kutonesha kidonda cha Simba aliyejeruhiwa na maaskari wa JWTZ, Green Warriors