JKT Ruvu yabadili jina
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Baada ya Shirikisho la soka nchini, (TFF) kuwataka wamiliki wa timu kuhakikisha timu zao hizo hazishiriki ligi moja na ikitokea hivyo basi moja wapo inaenguliwa, tayari Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limeanza kuachana na timu zake na kubakiwa na moja tu ambayo itashiriki Ligi Kuu ama Ligi Daraja la kwanza.
Jeshi hilo limetoa msimamo wake ambapo sasa timu ya JKT Ruvu iliyokuwa na maskani yake Mlandizi mkoani Pwani, na kuhamia Mlalakua Dar es Salaam, sasa timu hiyo imebadili jina na inaitwa JKT Tanzania FC, mmoja wa wasemaji wa jeshi hilo amesema kuwa nchi nzima timu inayomilikiwa na jeshi hilo ni hiyo tu.
Timu za Ruvu Shooting, JKT Mgambo, JKT Orjolo, JKT Kanemba, JKT Mlale na nyinginezo sasa zitasimamiwa na wananchi wa maeneo husika na si JKT tena kama ilivyozoeleka