Zanzibar noma kotekote, yatwaa ubingwa wa soka la ufukweni

Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam

Kama unadhani timu ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes ni wabaya kwenye soka la kawaida kama ilivyofanya kweli huko Kenya kwenye michuano ya Chalenji kwa kuingia fainali, basi jana kikosi cha timu ya taifa ya Zanzibar cha soka la ufukweni kimetwaa ubingwa wa michuano ya Copa Dar es Salaam baada ya kuishinda timu ya taifa ya Malawi mabao 3-2 kwenye mchezo wa fainali.

Mchezo huo ulifanyika katika fukwe za Coco Beach Dar es Salaam na Zanzibar ilionekana kutakata katika michuano hiyo tangia ilipoanza, michuano hiyo ilishirikisha timu za Tanzania bara, Uganda, Zanzibar na Malawi ambapo kikosi hicho kiliibuka kinara.

Mabingwa Zanzibar wamepata kikombe na medali ya dhahabu wakati Malawi wamepata medali ya Fedha, mshindi wa tatu, Tanzania bara ameambulia medali ya shaba

Mabingwa wa soka la ufukweni, Zanzibar

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA