SIMBA YAACHANA NA STRAIKA WA MSUMBIJI NA ZAMBIA
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Uongozi wa klabu ya Simba ya Dar es Salaam umesitisha mpango wa kuwasajili washambuliaji Antonio Dayo Domingues wa Ferreviaro De Beira ya Msumbiji na Jonas Sekuhawa kutoka Zambia.
Mwenyekiti wa kamati ya usajili Zachatia Hanspoppe amesema wameamua kusitisha mpango huo na sasa watamsajili mchezaji mmoja tu wa kigeni ambaye ni Asante Kwasi kutoka Lipuli ya Iringa.
Aidha Hanspoppe ambaye ni kapteni mstaafu wa Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ), amesema wachezaji Laudit Mavugo na Nicolaus Gyan hawataachwa isipokuwa Method Mwanjale ndiye aliyeachwa