Azam FC yapaa kileleni, Mghana wake ang' ara

Na Saida Salum. Dar es Salaam

Klabu bingwa ya soka Afrika mashariki na kati, Azam FC imekamata usukani wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara baada ya kuilaza Stand United mabao 3-0 mchezo ukimalizika usiku huu katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam.

Kwa ushindi huo mnono Azam inakaa kileleni mwa msimamo wa ligi, ikifanikiwa kufikisha alama 26 ikicheza mechi 12, Simba SC ndio walikuwa wakiongoza ligi hiyo, lakini inaweza kurejea kileleni endapo itashinda dhidi ya Ndanda FC.

Mabao ya Azam FC katika mchezo huo wa leo yamefungwa na Salmin Hoza, Benard Athur na Bruce Kangwa, ligi hiyo itaendelea kesho kwa michezo mitatu ambapo Mtibwa Sugar itawaalika Majimaji, Ndanda na Simba, wakati Lipuli ya Iringa itakuwa mwenyeji wa Prisons

Benard Athur raia wa Ghana amefunga goli la pili Azam ikishinda mabao 3-0

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA