Yanga yaipashia Reha FC kombe la FA
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam
Mabingwa wa soka nchini, Yanga SC jana wameendelea kujifua kwa ajili ya mchezo wao wa michuano ya Azam Sports Federation Cup, maarufu kombe la FA ambapo Jumapili ijayo itacheza na timu ya Reha FC inayoshiriki Ligi daraja la pili (SDL).
Katibu mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa amesema kikosi chake kipo tayari kwa mchezo huo na kinachompa jeuri ni kurejea uwanjani kwa wachezaji wake ambao walikosekana muda mrefu kutokana na majeruhi, Amissi Tambwe ni miongoni mwa wachezaji majeruhi wa muda mrefu ambapo sasa ataanza kucheza kwenye ahindano hilo la FA.
Pia nyota wengine kama Donald Ngoma, Thabani Kamusoko na Papy Kabamba Tshishimbi nao ni miongoni mwa wachezaji walioanza kuitumikia timu hiyo na huenda katika mchezo wao wa Ligi Kuu bara dhidi ya Mbao FC wakaanza