MEXIME ATAMBIA ATUPELE, ATHANAS
Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam
Kocha mkuu wa timu ya soka ya Kagera Sugar ya Misenyi Bukoba mkoani Kagera, Mecky Mexime ameonyesha kufurahishwa na safu yake mpya ya ushambuliaji kufuatia usajili uliofanywa na kikosi chake kwa Atupele Green na Pastory Athanas.
Akizungumza hivi karibuni mara baada ya usajili huo, Mexime amesema ana imani na ujio wa mshambuliaji Atupele Green na winga Pastory Athanas utawapa jeuri ya kufanya vizuri katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara na michuano ya kombe la FA.
Kocha huyo amedai, anawafahamu vema wachezaji hao ni wazuri na wataweza kuisaidia timu kuweza kupambana vikali kwenye ligi hiyo na huenda wakarejea kwenye nafasi za juu kama ilivyokuwa kwa msimu uliopita.
Atupele na Athanas wote kwa pamoja wameachwa na Singida United, Atupele amewahi kucheza Kagera Sugar, Coastal Union, Ndanda na Yanga, wakati Athanas amecheza Stand United, Simba SC na Singida United