JKU YAISHIKISHA ADABU ZIMAMOTO

Na Mwandishi Wetu. Zanzibar

Timu ya Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) jioni ya leo imefufua matumaini ya kusonga mbele katika michuano ya kombe la Mapinduzi baada ya kuilaza timu ya Jeshi la Zimamoto bao 1-0 mchezo wa kwanza kundi B na kujikusanyia pointi tatu muhimu.

Bao lililoipa ushindi JKU lilifungwa mapema kabisa na Salum Musa Bajaka katika dakika ya kwanza kabisa kuanza kwa pambano hilo, mechi nyingine ya pili inaendelea kupigwa usiku huu kati ya Mlandege na Taifa Jang' ombe uwanja huo huo wa Amaan, Zanzibar.

Michuano hiyo itaendelea tena kesho kwa kundi A, Azam Fc vs Mwenge utaanza saa 10:00 na kufuatiwa na mchezo mwingine kati ya Jamhuri na URA ya Uganda ambayo ni timu mwalikwa

Kikosi cha JKU kimeifunga Zimamoto 1-0

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA