Wanachama Yanga Mwanza wawajaza noti wachezaji kuiua Mbao kesho
Na Paskal Beatus. Mwanza
Wanachama na matawi yote wa klabu ya Yanga jijini Mwanza wamechangishana kiasi cha fedha shilingi Laki tisa na elfu thelasini na kumkabidhi kaimu mwenyekiti wa klabu hiyo Clement Sanga ili awapatie wachezaji wao kama motisha ya kuisambaratisha timu yao ya Mbao Fc ambao watakutana nao kesho Jumapili mchezo wa Ligi Kuu bara uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.
Wanachama hao wamekutana leo na kufanya kikao chao kilichoudhuriwa pia na kaimu mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga, na katika maadhimio hayo wanachama hao wameahidi kuchangishana fedha ili kusaidia usajili wa wachezaji kwa msimu ujao.
Yanga kwa sasa haina mfadhili hasa baada ya kujiuzuru kwa mwenyekiti wake Yusuf Manji ambaye pia alikuwa akijitolea kuisaidia timu hiyo, kesho Yanga itachuana na Mbao na tayari imewasili jijini humo kwa ndege ikitokea Dar es Salaam, ligi hiyo pia itaendelea kwa mchezo mwingine kati ya Njombe Mji na Singida United uwanja wa Sabasaba mjini Njombe