AZAM FC YAWALAMBISHA ICE CREAM, POLISI TANZANIA

Na Paskal Beatus. Dar es Salaam

Mabingwa wa soka wa kombe la Kagame, Azam FC usiku huu imeifunga bila huruma timu ya maafande wa Jeshi la Polisi Tanzania kwa mabao 3-1 mchezo wa kirafiki uliofanyika uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Polisi Tanzania ambayo Jumapili iliyopita iliilazimisha sare tasa 0-0 mabingwa wa soka nchini Yanga, leo wameshindwa kufurukuta mbele ya wauza Ice cream hao wa Bakhresa, Polisi walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa kipindi cha kwanza na kwenda mapumziko wakiwa mbele.

Kocha wa Azam alifanya mabadiliko kipindi cha pili kwa kuwaingiza Peter Paul na Waziri Junior, mabadiliko yaliyozaa matunda kwani Paul alifunga mawili na Junior akafunga lingine moja la ushindi, huo ni ushindi wa tatu mfululizo kwa Azam baada ya kuifunga Mvuvumwa 8-1, Villa Squad 7-1 na leo 3-1 dhidi ya Polisi Tanzania

Azam FC imefunga Polisi Tanzania jana

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA