TAMBWE ASEMA BADO MBAO FC
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam
Mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Amissi Tambwe amesema baada ya kuwatungua Reha FC katika mchezo wa kombe la Azam Sports Federation Cup, (ASFC) maarufu kombe la FA, amesema bado Mbao FC ambao nao amepanga kuwanyoosha Jumamosi ijayo.
Tambwe alikuwa majeruhi kwa muda mrefu lakini juzi alirejea uwanjani na kuiwezesha timu yake ya Yanga kuilaza Reha FC mabao 2-0 uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, timu hizo zilienda kupumzika zikiwa hazijafungana hata bao, lakini kipindi cha pili Yanga walipata mabao hayo mawili yaliyofungwa na Pius Buswita na Tambwe.
Kwa Amissi Tambwe hilo lilikuwa bao lake la kwanza msimu huu na pia ulikuwa mchezo wake wa kwanza tangia apone majeraha yake yaliyomweka benchi kwa muda mrefu, katika mazungumzo yake, Tambwe amesema ataendelea kufunga karibu kila mechi na hakuna wa kumzuia