Mkuu wa mkoa Dar es Salaam, apewa shavu Yanga
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam
Aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Said Meki Sadiki ameteuliwa kuwa mjumbe kwenye kamati mpya iliyoundwa kuelekea katika mfumo wa mabadiliko utakaoifanya klabu hiyo kuwa kampuni ya kuuza Hisa kama ilivyo kwa watani zao Simba SC.
Mwanasheria Alex Gaitani Mgongolwa amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa kamati hiyo iliyowahusisha wataalamu wa sheria na uchumi, Profesa Mgongo Fimbo naye amechaguliwa kuwa mjumbe wa upande wa masuala ya katiba wakati Mohamed Nyenge anakuwa mjumbe masuala ya uchumi na fedha, George Fumbuka, Masuala ya uwekezaji na mshauri wakati Felix Mlaki, uchumi na fedha.
Meki Sadiki mbali na kuongoza mkoa wa Dar es Salaam wakati wa utawala wa awamu ya nne ya Jakaya Kikwete, akaongoza pia mkoa wa Kilimanjaro katika utawala wa awamu ya tano ya John Pombe Magufuli kabla ya kustaafu.
Klabu ya Yanga inatarajia rasmi kuingia kwenye soko la Hisa na kuna uwezekano mkubwa timu hiyo ikaangukia kwa bilionea ambaye atanunua Hisa asilimia 49 na asilimia 51 zitabaki kwa wanachama