MLANDEGE YAILAZA JKU 2-1, MWENGE NAO WATAKATA

Na Mwandishi Wetu. Zanzjbar

Timu ya Mlandege mchana wa leo imeanza vema michuano ya Mapinduzi baada ya kuilaza timu ngumu ya JKU mabao 2-1 uwanja wa Amaan, Zanzibar huo ulikuwa mchezo wa ufunguzi.

Mlandege ilicheza vizuri na kujipatia mabao yake kupitia kwa Khamis Abuu dakika ya 18 na Abubakar Ame (Luiz) dakika ya 60, goli la JKU limefungwa na Khamis Abdallah dakika ya 34.

Timu ya Mwenge kutoka Pemba iliwachapa ndugu zao Jamhuri kwa bao 1-0 lililofungwa na Ally Salim Bajaka kunako dakika ya 31, mechi nyingine inapigwa usiku huu kati ya Taifa Jang' ombe na Zimamoto, michuano hiyo itaendelea tena kesho ambapo Zimamoto watacheza na JKU na Taifa Jang' ombe na Mlandege

Michuano ya Mapinduzi imeanza leo uwanja wa Amaan, Zanzibar

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA