SIMBA YACHANUA MAKUCHA NA KUIPALULA NDANDA FC

Na Ikram Khamees. Mtwara

Simba Sc jioni ya leo imefufua tena mbio zake za ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara baada ya kuilaza Ndanda Fc "Wanakuchele" nyumbani kwao katika uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.

Hadi mapumziko timu hizo hazikufungana hata bao, kipindi cha pili Simba walikuja na kasi mpya na kulisakama lango la Ndanda kama nyuki na kuweza kujipatia mabao hayo mawili yote yakifungwa na mshambuliaji John Raphael Bocco "Adebayor" dakika ya 52 na 56.

Kwa ushindi huo Simba inarejea kileleni ikifikisha pointi 26 sawa na Azam Fc ila inazidi kwa magoli ya kufunga, Lipuli Fc ya Iringa ilikubali kichapo nyumbani baada ya kufungwa 1-0 na Tanzania Prisons uwanja wa Samora mjini Iringa, Mtibwa Sugar nayo ikicheza nyumbani Manungu Complex, Morogoro imeifunga 2-1 Majimaji ya Songea uwanja wa Manungu Complex, Morogoro

Simba imeifunga Ndanda 2-0 leo

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA