Mpiga picha wa Azam Media afariki
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam
Mpiga picha wa televisheni wa kituo cha Azam Tv, Iddy Salum "Mambo" amefariki dunia leo akiwa hospitalini jijini Mwanza alipokuwa akitibiwa.
Idd alikuwa maarufu na kamera yake pembeni ya goli wakati kituo hicho kikirekodi mchezo wa Ligi Kuu au nashindano yoyote yanayorushwa na Azam Tv.
Mpiga picha huyo mara kwa mara amekuwa akikaa upande wa karibu na vyumba vya kubadilishia jezi wachezaji, mbali na kupiga picha, marehemu pia alikuwa mwandishi wa Azam Media.
Mungu amweke mahara pema peponi, Amina