MAPINDUZI CUP KUANZA KUTIMUA VUMBI KESHO
Na Mwandishi Wetu. Zanzibar
Michuano ya kombe la Mapinduzi inatarajia kuanza kutimua vumbi kesho katika uwanja wa Amaan, Zanzibar kwa mechi tatu, timu za Mlandege FC na JKU zitaanza kuchuana kuanzia saa 8:00 mchana, ikifuatiwa na mechi nyingine kati ya Jamhuri na Mwenge zote za Pemba mchezo wao ukipigwa saa 10:00 jioni.
Mchezo mwingine utapigwa usiku kuanzia saa 2:15 kati ya Taifa Jang' ombe na Zimamoto, michuano hiyo inayoshirikisha pia miamba ya soka nchini Simba na Yanga pamoja na Singida United.
Michuano hiyo inayoratibiwa na chama cha soka Zanzibar, (ZFA) itaendelea kutimua vumbi, lakini Siku ya Jumapili Azam FC itaumana na Mwenge, wakati Singida United itacheza na Zimamoto, siku ya Jumanne Simba itacheza na Mwenge wakati Yanga itachuana na Mlandege.