KITAELEWEKA LEO YANGA NA MBAO CCM KIRUMBA
Na Paskal Beatus. Mwanza
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara inaendelea tena leo kwa mitanange miwili kupigwa katika viwanja viwili tofauti, lakini nchi itasimama kwa muda pale jijini Mwanza kwenye uwanja wa CCM Kirumba wakati Mbao Fc itakapowaalika mabingwa watetezi Yanga Sc.
Kocha wa Mbao Fc, Mrundi, Etiene Ndayiragije ametamba kuendeleza kichapo kwa Yanga kwani msimu uliopita Mbao iliifunga Yanga bao 1-0 kwenye Ligi Kuu bara na pia kwenye kombe la FA, hivyo leo tena Mbao anashinda, lakini kocha msaidizi wa Yanga Shadrack Nsajigwa "Fuso" amesema thubutuu!.
Nsajigwa beki wa zamani wa kikosi hicho pamoja na timu ya taifa, Taifa Stars ametamba kulipiza kisasi katika mchezo wa leo huku akidai ilichokipata Reha Fc ndicho itakipata Mbao Fc leo na shahidi ya hayo ni dakika 90