Hatimaye George Weah awa Rais wa Liberia

Tume ya taifa ya nchini Liberia imemtangaza rasmi mwanasoka wa zamani wa AC Milan na Mwafrika pekee kushinda tuzo ya Ballon' D'Or, George Opong Weah baada ya kupata ushindi mkubwa kwenye uchaguzi wa taifa hilo.

Weah anakuwa Rais wa 25 na amemshinda Joseph Boakai ambaye alikuwa makamu wa Rais wa nchi hiyo, mwanasoka huyo bora wa dunia aliyepata pia kuzichezea Monaco, Marseile zote za Ufaransa, Inter Milan ya Italia, Manchester City na Chelsea zote za England, ameibuka mshindi katika majimbo 12 kati ya 15.

Aidha Weah ambaye aliwahi kuja nchini Tanzania akiwa na timu ya taifa ya Liberia, amewashukuru wananchi wa taifa hilo waliomchagua na kuahidi kuleta mapinduzi makubwa, Weah aliwahi pia kushinda urais wa nchi hiyo lakini matokeo yalifutwa na mahakama

George Weah Rais mpya wa Liberia

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA