MO KUMSHUSHA KOPUNOVIC AKIKABIDHIWA TIMU
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Kuna uhakika mkubwa kuwa aliyekuwa kocha mkuu wa Simba SC, Goran Kopunovic akarejea tena Msimbazi kama kukinoa kikosi hicho kilichotangaza kuachana na kocha wake mkuu Mcameroon, Joseph Omog kufuatia mwenendo mbaya hadi kutolewa mapema katika michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) maarufu kombe la FA.
Simba iliondoshwa na timu ya daraja la pili ya Green Warriors ya Mwenge na kuvuliwa ubingwa, Simba ilifungwa mabao 4-3 kwa mikwaju ya penalti baada ya sare ya 1-1 ndani ya dakika 90, baada ya kuondoka Omog, Simba sasa inempa jukumu kocha wake msaidizi Masoud Djuma raia wa Burundi na kocha wa makipa Muharami Mohamed "Shilton".
Lakini kuna taarifa njema kuwa mshindi wa zabuni mfanyabiashara, Mohamed Dewji "Mo" ambaye ameshinda zabuni na kununua Hisa asilimia 51za klabu hiyo ana mpango wa kumrejesha kazini kocha Goran Kopunovic ambaye aliwahi kuinoa Simba na kuipa kombe la Mapinduzi, Mo atamrejesha kocha huyo pindi atakapopewa rasmi mamlaka ya kuiendesha timu hiyo kama mwekezaji mwenye nguvu