Milambo FC yatupwa nje kombe la FA

Na Emil Kasapa. Tabora

Timu ya Milambo Fc ya Tabora imeondolewa katika hatua ya pili ya michuano ya kombe la shirikisho nchini baada kufungwa kwa penati 3-1 na timu ya Buseresere ya GEITA mara baada ya sare ya bao mbili kwa mbili ndani ya dakika 90.

Salum Moshi alikuwa wa kwanza kuifungia Buseresere dk ya  19 kabla ya Shaban Madanganya kusawazisha dk ya 44.
Kipindi cha pili Abuu wakati alijifunga dk 67 kabla ya Peter Croach kusawazisha dk ya 75.

Milambo walipata penati kupitia kwa Yohana John wakati Lucas Misana,Rashid Kopa na Fidelai Philimon wote walikosa

Kwa upande wa Buseresere walipata kupitia kwa Aman Abud ,Nicholous Samwery na Kassim Ibrahim wakati Juma Nade na Lameck Masabo walikosa mikwaju yao ya penati.

Kesho katika uwanja wa Mwinyi Rhino watacheza na Alliance ya mwanza katika mwendelezo wa mashindano hayo.

Milambo imetupwa nje kombe la FA

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA