SIMBA YAVULIWA UBINGWA WA FA, YAPIGWA NA KITIMU CHA DARAJA LA PILI

Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam

Mabingwa watetezi wa kombe la Azam Sports Federation Cup (ASFC) maarufu kombe la FA, Simba SC usiku huu wamevuliwa ubingwa na timu ya daraja la pili ya Green Worriors kwa mabao 4-3 kwa mikwaju ya penalti kufuatia sare ya bao 1-1 ndani ya dakika 90.

Mchezo wa ufunguzi kwa mabingwa hao watetezi uliofanyika uwanja wa Azam Complex, Chamazi, na vijana wa Green Worriors kulitia msukosuko lango la Simba mara kwa mara, Hussein Bunu alitangulia kuifungia Worriors bao la kuongoza kipindi cha kwanza, kabla ya John Bocco "Adebayor" kuisawazishia Simba kwa penalti.

Hadi mpira unamalizika timu hizo zilikuwa sare 1-1, na ndipo zilipoelekea katika mikwaju ya penalti ambapo Simba imetupwa nje huku vijana wa Green Worriors wakitinga hatua ya 32 bora, kesho uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, Yanga SC watacheza na Reha FC

Simba SC imevuliwa ubingwa wa FA leo

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA