Yanga yachomoza CAF kwa ubora wa kandanda Afrika
Na Saida Salum. Dar es Salaam
Shirikisho la kandanda barani Afrika, CAF, limetaja viwango vipya vya ubora wa kandanda kwa vilabu huku timu ya Esperance ya Tunisia ikiongoza, katika toleo lao lililochapishwa hivi karibuni limeziweka pia klabu tatu za Tanzania ambazo ni Yanga, Azam na Simba.
Yanga SC ambao mwakani watashiriki michuano ya Caf ikicheza Ligi ya mabingwa, inaongoza katika viwango hivyo kwa upande wa timu za Tanzania ikishikilia nafasi ya 345 ikifuatiwa na Azam FC iliyo katika nafasi ya 365.
Wekundu wa Msimbazi ambao na mwakani watashiriki michuano inayoandaliwa na Caf ya kombe la Shirikisho, yenyewe inakamata nafasi ya 371, hata hivyo Simba haikupata nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa kwa kipindi cha miaka minne jambo ambalo limepelekea timu hiyo iliyowahi kuingia fainali ya kombe la Caf mwaka 1993 kushuka