MTANGAZAJI MAARUFU WA MICHEZO AFARIKI DUNIA
Na Saida Salum. Dar es Salaam
Tasnia ya habari leo imepatwa na msiba mzito baada ya aliyekuwa mtangazaji maarufu wa kipindi cha michezo cha redio Uhuru, Limonga Justine Limonga kufariki dunia.
Marehemu alikuwa akitangaza kipindi cha michezo kinachorushwa na redio Uhuru kuanzia saa 1:00 usiku hadi saa 1:30 usiku.
Marehemu aiingia kwenye utangazaji baada ya kuachana na kutuma salamu ambayo ilimsukuma hadi kuwa mtangazaji, bado tutaendelea kuwajuza taarifa za msiba wake kama mazishi yatafanyika lini na wapi.
Kwa niaba ya Mtendaji mkuu wa Mambo Uwanjani inawapa pole wafiwa kwa msiba huo pamoja na Radio Uhuru Fm