Simba kurejea kileleni leo?

Na Ikram Khamees. Mtwara

Wekundu wa Msimbazi,Simba Sc jioni ya leo itakuwa ugenini kwa Ndanda Fc uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara, Simba iliwasili mjini Mtwara Alhamis ikitokea Dar es Salaam ambako ina kumbukumbu ya kuvuliwa ubingwa wa kombe la FA.

Mchezo huo wa leo utakuwa mgumu kutokana na kila timu kutaka pointi tatu muhimu, wenyeji Ndanda wao walibadili nahodha kuelekea mchezo huo ambapo jukumu zima alikabidhiwa mshambuliaji Jacob Masawe na kiungo wa zamani wa Yanga, Salum Telela.

Simba nao wameamua kubadili benchi la ufundi, ikimtoa Mcameroon, Joseph Omog na kumpa Mrundi, Masoud Djuma, endapo Simba itashinda mchezo huo itarejea kileleni kwani jana usiku Azam Fc ilishinda mabao 3-0 na kukamata usukani

Simba wanaweza kurejea kileleni leo

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA