TAMBWE AREJEA NA MABAO YAKE, YANGA IKIIFINYANGA REHA FC 2-0

Na Ikram Khamees. Dar es Salaam

Klabu bingwa ya soka Tanzania bara, Yanga SC jioni ya leo imefanikiwa kutinga hatua ya 32 bora ya kombe la Azam Sports Federation Cup (ASFC) maarufu kombe la FA baada ya kuilaza Reha FC ya Chang' ombe mabao 2-0 uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Vijana wa Reha waliidhibiti Yanga hadi mapumziko wakienda sare tasa 0-0, kipindi cha pili Reha FC nao walilitia msukosuko lango la Yanga na kuambulia kupata kona mbili mfululizo ambazo hazikuzaa matunda.

Kocha msaidizi wa Yanga shadrack Nsajigwa "Fuso" alijaribu kubadili kikosi angalau kupata bao la kuongoza na la ushindi.

Yanga waliamka dakika za mwishoni na kujipatia mabao yake mawili kupitia kwa Pius Buswita na Amissi Tambwe ambao ni mchezo wake wa kwanza tangu arejee uwanjani.

Juzi watani zao Simba SC ilivuliwa ubingwa wa michuano hiyo baada ya kufungwa na timu ya daraja la pili ya Green Warriors mabao 4-3 kufuatia sare ya bao 1-1 ndani ya dakika ya 90

Amissi Tambwe amerejea kwa kasi ile ile ya kufunga

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA